Kwa vile hupati taarifa za mara kwa mara kutoka kampuni ya Nokia haimaanishi kuwa kampuni hiyo ndio imekufa. Nokia bado iko katika biashara na kwa sasa ina mipango kadha wa kadha ili kuhakikisha inarudi kwa kishindo.
Kampuni hiyo baada ya kuuza biashara yake ya simu kwa Microsoft ilisema kuwa itarudi katika soko la simu miaka ya baadae na sasa kwa kuwa tayari Microsoft ruhusa yao ya kutumia jina la Nokia kwenye simu imeshapita (expire) basi wanaweza kutoa tena simu zao kama zamani. Inasemekana itarudi kwa kutoa simu kadhaa ambazo zinaweza zikawa zinatumia programu endeshaji ya Android!
Ukiachana na ujio wake bado kampuni linaonyesha uwezo mkubwa wa kujiamini, hii imepelekea mpaka kampuni hilo kuweka nia ya kulinunua kampuni la Withings kutoka Ufaransa
Kampuni hili litanunuliwa kwa takribani dola milioni 191 za kimarekani. Kwa kuwa kampuni la Withings inajihusisha na mambo (vifaa) vya kidigitali katika kujiweka fiti (mazoezi), hii inaweza ikawa ni njia moja wapo kwa Nokia katika kuingia katika teknolojia ya kidigitali ya kuweka afya fiti.
Ukiachana na Nokia kampuni la Withings kwa muda murefu imejihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kujiweka fiti kama vile WiFi Body Scale, Tracker ya E-ink, themometa ya kutumia Bluetooth, Saa janja ijulikanayo kama Activité
Mkurugenzi mkuu wa Withings, Cédric Hutchings amesema kuwa “Mipango yetu na ile ya Nokia inaendana sambamba kabisa katika kuhakikisha watu wanapata bidhaa nzuri za kujiweka fiti”
Hapo inaonekana dhahiri kuwa makampuni yote mawawili yana nia moja katika ufanyaji kazi wao.
Ripoti zilizopo zinasema kuwa dili hilo litatiwa saini na kumalizika katikati ya mwaka huu (2016). Withings ina wafanyakazi 200 ambao baada ya kusainiwa kwa dili hili watakuwa chini ya Nokia Technologies.
Katika sehemu ya comment hapo chini niandikie hii unaipokea vipi kutoka kampuni la Nokia. Na je unahisi kampuni hilo limeshakufa kabisa au bado linaweza kurudi sokoni na kurudisha hadhi yake ya zamani?