Xiaomi licha ya kuwa kampuni lenye jina kubwa sana katika soko la china la simu, bado kampuni inajiendeleza kwa kiasi kikubwa. Sasa wanakuja na teknolojia ya saa janja na hivi sasa wamejikita na saa janja kwa ajili ya watoto
Saa janja sawa sio kitu kipya lakini tujaribu kuona Xiaomi watakuwa wamewaandalia nini watoto kupitia kifaa chake hichi?
Saa hii imetengenezwa vizuri ndani yake ina huduma ya GPS ambayo inaweza wapa mwangaza wazazi katika kujua maeneo ambayo watoto wao wapo. Cha kuvutia zaidi ni kwamba mzazi anaweza seti eneo husika ambalo mwanae akitoka nje ya eneo hilo mzazi anaweza pata taarifa haraka.
Watoto wanaweza wakapokea na kupiga simu kupiti saa hii kama zilivyo saa janja zingine. Vile vile wanaweza wakabonyeza kibonyezo cha SOS kukiwa na dharura. Kwa kubonyeza kibonyezo hiko saa itaweza kurekodi sauti kwa sekunde 7 na kujituma kwa simu ya mzazi. Sauti hiyo itajituma ikiwa imeambatana na taarifa za eneo ambalo saa hiyo (mtoto) ipo
Saa janja hiyo inaruhusu huduma za WiFi na Bluetooth. Katika swala zima la kupiga simu, saa inakuja na eneo la kuweka laini
Kwa matumizi ya kawaida saa hii inaweza ikakaa kwa muda wa siku mbili kwani inakuja na betri la uwezo wa mAh 300.
Saa hii inaweza ikatumika sambamba kwa kutumia simu janja ambazo zinatumia program endeshaji ya Android 4.2 na kuendelea, iOS 8 na kuendelea. Pia saa hii sio kwamba itatumika kwa vifaa vya Xiaomi tuu
Saa janja hii kwa jina lingine inafahamika kama MituWatch.