Ukuaji wa sayansi na teknolojia ya matibabu yazidi kufika mbali, madaktari nchini Marekani wafanikiwa kwa mara ya kwanza kabisa nchini humo kufanya oparesheni ya kuunganisha kiungo cha siri cha mtu aliyefariki kwenda kwa mtu mwingine.
Bwana Thomas Manning wa jimbo la Massachusetts nchini marekani alipoteza sehemu zake za siri (penis) mwaka 2012 baada ya kugundulika ya kwamba kulikuwa na saratani (cancer) iliyokuwa inajengeka kwenye eneo hilo. Hili lilipelekea yeye kukatwa sehemu yake ya siri.
Bwana Thomas ambaye hajawa na mpenzi kwa muda mrefu sasa amesema ilikuwa ni shida kujaribu kuanzisha uhusiano na mwanamke na kisha kumwambia ya kwamba yeye ni kilema kwenye sehemu za siri. Hili lilimfanya iwe vigumu kuanzisha mahusiano, na sasa anafuraha hilo litawezekana kwa sasa.
Inasemekana oparesheni hiyo ilichukua muda wa masaa 15 kufanyika (Mei 8 na 9), na iliwachukua madaktari waliohusika miaka 3 kujifunza na kujiandaa kwa kufanyika kwa oparesheni hiyo.
Hadi sasa wamesema oparesheni hiyo imefanikiwa kwani kila kitu kinafanya kazi kama kinavyotakiwa kwa Bwana Thomas. Mishipa ya damu na ya ‘nerve’ yote imeunganishwa vizuri, hakuna dalili yeyote ya matatizo.
Wanasayansi wanategemea kwa kutumia teknolojia za kisasa muda si mrefu watakuwa na uwezo wa kutengeneza viungo muhimu vya mwili kupitia njia za ‘labaratory’. Wakifanikiwa katika teknolojia hii inamaanisha wagonjwa wanaosubiria viungo vya mwili hawataitajika kusubiria watu wengine kufa tena.
Oparesheni ya kwanza kabisa ya kiungo cha siri cha mwanaume ilifanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2014, kwa kijana ambaye kiungo chake hicho kilikuwa kimeharibiwa kutokana na tohara ambayo haikufanywa vizuri. Kijana huyo alipona na sasa ana hadi mtoto.