fbpx

Uwezekano wa kuibiwa nywila za iOS na Mac kwa kutumia ‘Image file’ yenye kirusi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Tafiti za Cisco imeonyesha uwezekanano wa vifaa vinavyotumia iOS na Mac kudukuliwa kwa kutumia file lililo katika mfumo wa picha la lenye kirusi.

Utafiti huo umebainisha kuwa file lililo katika mfumo wa TIFF linaweza likatumwa kwa njia ya MMS, barua pepe au likawekwa kwenye tovuti fulani halafu mtu akaongozwa kutembelea tovuti hiyo. Mbaya zaidi ni kwamba file hilo lina uwezo wa kuficha virusi na kuathiri kifaa chako bila kujua.

Baadhi ya vifaa vinavyotengenezwa na Apple(kampuni)

Nywila ni kitu muhimu sana katika ulimwengu wa kidijitali hivyo ni lazima kutumia nenosiri ambalo itakuwa ni ngumu mtu mwingine kubashiri.

Aidha udhaifu huo unampa uwezo mdukuzi kuweza akafanya kila kitu hata akiwa mbali na kifaa hicho iwapo anakuwa ameweza kudukua kifaa chako; iwapo ameweza kupata password na username yako unayotumia na hivyo kuweza kupata idhini ya kuona na kufanya kila kitu kwenye kompyuta/iPad.

Kompyuta aina ya Mac

Kompyuta aina ya Mac: Moja ya bidhaa ghali kutoka Apple.

Tayari wahusika wamesharekebisha udhaifu huo ambao uliibuliwa na mtafiti kutoka Cisco na ili kifaa chako kiweze kuwa katika usalama inabidi kufanya masasisho ya programu endeshaji kuja kwenye toleo la karibu kwenye vifaa vyote kutoka Apple.

INAYOHUSIANA  Space X kazini tena, Safari hii wachemka

Ni matumaini yetu makala hii itakusaidia ili kuweza kuzuia kifaa chako kisidukuliwe. Kama kawaida yetu TeknoKona tupo na wewe kiteknolojia zaidi.

Vyanzo: TechJuice, EveningStandard, TnW

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.