fbpx

Android, Nokia, simu, Uchambuzi

Hili ndio toleo la Nokia 7

hili-ndio-toleo-la-nokia-7

Sambaza

Simu za Nokia ambazo zinaendeshwa na programu endeshaji ya Android zinaendelea kupendwa na kwa sehemu zingine kama Uchina zimejichukulia umaarufu mkubwa.

Matoleo mengi ya Nokia yapo madukani lakini Nokia 6 ambayo ilizinduliwa huko Uchina na kuacha historia ambayo itakumbukwa kwa miaka mingi tu na kampuni husika, soma zaidi hapa.

Hii ni Nokia 7 na ina haya yafuatayo:-

Kioo & Kamera. Kioo chenye ukubwa wa inchi 5.2, ubora wa picha ukiwa 1080*1920 pixels lakini ikiwa inakingwa Corning Gorilla Glass 3 isipate madhara inapoanguka. Upande wa kamera ya nyuma ina MP 16 na ile ya mbele ina MP 5 iliyotengenezwa na Zeiss ikiwa na LED flash mbili.

INAYOHUSIANA  Google Classroom yaboreshwa

Programu endeshi & Prosesa. Imewekwa Android 7.1 lakini ikiwa na uwezo wa kuhamia Android 8 (Oreo). Prosesa ambayo ipo kwenye Nokia 7 ile maarufu na inayotumiwa na makampuni mengi tu, Qualcomm SDM630 Snapdragon 630 kasi yake ikiwa Octa-core 2.2 GHz.

toleo la Nokia 7
Nokia 7 inatumia laini 2 za simu na ikipatikana katika rangi mbili; Nyeupe na Nyekundu.

RAM & Diski uhifadhi. Moja ya kiungo muhimu cha kufanya simu kutokwamakwama ni RAM, Nokia 7 ina GB 4 na GB 64 uhifadhi wa ndani kwenye simu lakini ikiwa na uwezo wa kukubali uhifadhi wa ziada wa mpaka GB 256.

INAYOHUSIANA  Uwezo wa kumuongeza mtu kwenye kundi la WhatsApp bila Admin kujua

Betri & Sifa nyinginezo. Hapa kuna betri yenye 3000 mAh aina ya Li-ion ambalo halitoki; linadumu kwa chaji saa 340 ukitumia kwenye intateti tu, saa 15 (kuongea+intaneti), saa 85 ukitumia kusikiliza muziki peke yake.

Nokia 7 ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole iliyowekwa upande wa nyuma, kuna redio, WLAN, Bluetooth, sehemu ya kuchomekea spika za masikioni, GPS, NFC.

toleo la Nokia 7
Nokia inakubali teknolojia za mawasilaiano kama vile GSM / CDMA / HSPA / EVDO / LTE.

Nokia 7 ipo madukani muda mrefu tu na kwa makadirio ni zaidi ya Tsh. 655,00. Nokia 7 Plus, 7.1, 7.1 Plus zipo na zinawika kweli. Uchambuzi wake utakuja katika siku za usoni.

Vyanzo: GSMArena, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Hili ndio toleo la Nokia 7 – TeknoKona Teknolojia Tanzania
    June 19, 2018 at 5:31 pm

    […] post Hili ndio toleo la Nokia 7 appeared first on TeknoKona Teknolojia […]