Nokia kurudi na simu janja zinazotumia Android – Je upo tayari kutumia tena?

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Enzi za kuchaji simu mara moja au mbili tuu kwa wiki, enzi za kutoshtuka kivile pale simu inapodondoka…. Watumiaji wapya wa simu watakuwa hawaelezi haya ila wale waliokuwa na simu tokea enzi za miaka ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 basi wanaelewa hizi ni baadhi ya sifa kubwa kwa simu za Nokia enzi hizo.

Nokia kuja na simu

Tulishaandika kuhusu mwisho wa Microsoft kuwa na hakimiliki la jina la Nokia katika biashara za simu, hakimiliki hiyo waliipata pale waliponunua kitengo cha biashara za simu kutoka kampuni ya Nokia Corporation mwaka 2014.

INAYOHUSIANA  OFA: Mohamed Salah akifunga goli tu, watu wanapata muda wa maongezi wa dakika 11 bure

Kilichotokea

  • Microsoft baada ya kununua biashara za simu za Nokia taratibu waliacha kutumia jina la Nokia na kutumia Microsoft Mobile kama sehemu ya makubaliano yao
  • Kipindi chote cha mpito kampuni ya Nokia Corporation hawakutakiwa kuanzisha biashara ya simu zingine kwa kutumia jina la Nokia
  • Na sasa hakimiliki ya jina hilo kwenye biashara za simu imerudi kwa Nokia Corporation

Kampuni ya Nokia Corporation kupitia kitengo chao kinachosimamia biashara na teknolojia za simu cha Nokia Technologies wameingia makubaliano na kampuni ya HMD Global, HMD watatengeneza na kuuza simu zinazobeba jina la Nokia.

INAYOHUSIANA  Google yaongeza mbwembwe kwenye Gmail

Katika makubaliano hayo HMD Global wamepewa hakimiliki ya kutengeneza simu janja zitakazokuwa zinatumia jina la Nokia na huku Nokia wenyewe wakihusisha kwenye masuala yote ya ubora wa simu hizo. HMD Global wamesema ni lengo lao kuhakikisha simu na tableti watakazozileta zinaendane na hadhi kubwa ya jina la Nokia.

Nokia watanufaika kivipi?

Nokia watapata malipo ya mara kwa mara kupitia haki miliki ya jina hilo, pia watapata malipo mengine kutokana na teknolojia zao zitakazotumika kwenye simu hizo.

Kwa kiasi kikubwa Nokia bado wanaingiza pesa nyingi kila mwaka kutoka makampuni yote ya utengenezaji simu kutokana na teknolojia zao kadhaa za mawasiliano zinazotumika kwenye simu karibia zote.

Wamesema simu zote zitakazokuja zitakuja na programu endeshaji ya Android.

INAYOHUSIANA  Fahamu Kuhusu Viatu Janja Kutoka Lenevo! #Teknolojia

Tuambie je kama simu zitakuwa na uwezo mzuri na kwa bei nzuri je utajisikia furaha kununua simu ya Nokia badala ya kampuni nyingine ya simu?

[socialpoll id=”2360696″]

Chanzo: Nokia

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |