Kipakatalishi: Ifahamu Lenovo ThinkPad X390

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ingawa simu zetu zinaweza kutumika kama ngamizi/kompyuta lakini bado kuna umuhimu wa kuwa na bidhaa hiyo ili kufanikisha shughuli za kila siku kwa urahisi na haraka zaidi kulingana na ufanisi wa bidhaa husika.

Iwapo utazungumzia vipatalishi vyembamba ambavyo vinatengenenezwa na makampuni makubwa duniani itakuwa si kitu cha ajabu sana kuona Lenovo ikionekana kwenye orodha na hii inatokana na kwamba kampuni hiyo imekuwa ikitoa kompyuta nyembamba lakini pia zenye uwezo wa hali ya juu.

Kwenye onyesho la MWC 19 lililofanyika mapema mwaka huu kampuni hiyo iliweza kutangaza kuhusu bidhaa yao, Lenovo ThinkPad X390 ambayo sasa imeweza kuzinduliwa na sifa zake kuweza kufahamika kinagaubaga:

INAYOHUSIANA  Biashara ya kwanza kufanyika mtandaoni

Kipuri mama/Muonekano: Kipakatalishi hicho ni chembamba inchi 13.3 ikiwa ni nyembamba kwa 12% zaidi kwa mtangulizi wake (Lenovo ThinkPad X380 Yoga), kuna toleo lenye kioo cha mguso/kisichokuwa cha mguso. Kipuri mama kilichotumika huko ni  kizazi cha nane Intel® Core™ i7. Upande wa kipuri cha picha ni Intel HD Graphics 620.

Diski uhifadhi/RAM: Kompyuta hiyo inakubali RAM za DDR4 mpaka GB 32 zenye kasi ya 2400GHz. Upande wa memori ya ndani (SSD) ni GB 512/TB 1.Lenovo ThinkPad X390

INAYOHUSIANA  Angani kwa siku tano kwenye ndege ya abiria

Kamera/Ulinzi: Kuna wale ambao wanapenda kuchungulia kile unachofanya kwenye kompyuta, sasa kwenye Lenovo ThinkPad X390 imewekwa mfuniko wa mpira kwenye kamera husika kwa lengo la kuzuia kwa yeyote atakayejaribu kutaka kuchungulia. Inatoa mlio iwapo itagundua kuna mtu anajaribu kuangalia/kuchungulia.

Uwezo wa betri: Kipakatalishi hicho betri yake ina uwezo wa kutunza umeme kwa saa 17.6; kwa teknolojia ya kuchaji haraka (65W) inachukua saa moja kujaza betri kwa 80% .

Mengineyo

Ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole kwa ajili ya ulinzi zaidi, inatumia Windows 10 Pro 64-bit, Inaweza kukamata 4G LTE, teknolojia ya Wi-Fi 6, 2*2 Wi-Fi, NFC, uzito wake unaanzia Kg 1.29.

Lenovo ThinkPad X390

Sehemu za kuchomeka vitu mbalimbali kwenye Lenovo ThinkPad X390.

Bei yake inaanzia $1,381|zaidi ya Tsh. 3,176,300 huku bei ikiongezeka kulinana na ukubwa wa RAM/diski uhifadhi utakaotaka, bei kubwa zaidi ni $2,001|zaidi ya Tsh. 4,602,300.

Vyanzo: Lenovo, Neowin

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.