fbpx
Afrika, Huawei, Udukuzi, Usalama

WSJ: Wafanyakazi wa Huawei wanahusika na udukuzi wa wanasiasa Afrika. #Skendo

huawei-wanahusika-na-udukuzi-wa-wanasiasa-afrika
Sambaza

Gazeti mashuhuri la nchini Marekani, Wall Street Journal katika uchunguzi wao wamebaini wafanyakazi wa Huawei wanahusika na udukuzi na kusaidia shughuli za kijasusi dhidi ya wanasiasa barani Afrika.

Wafanyakazi wa Huawei wanahusika na udukuzi wa wanasiasa Afrika
WSJ: Wafanyakazi wa Huawei wanahusika na udukuzi wa wanasiasa Afrika

Katika uchunguzi wao wamesema wamepata uhakika zaidi hasa kwenye mataifa kama Uganda na Zambia. Wamesema uchunguzi wao haujapata uhakika kama viongozi wa juu wa kampuni hiyo makao makuu wanafahamu kuhusu yale yanayofanywa na wafanyakazi wao katika nchi hizo.

INAYOHUSIANA  Wadukuzi wa Urusi wafichua nyaraka za Wanamichezo maarufu duniani

Shutuma za gazeti hilo zinasema wafanyakazi wa Huawei wamekuwa wakitoa msaada wa serikali kufuatilia mawasiliano ya wapinzani wao kisiasa kupitia teknolojia za mawasiliano ya simu, hii ikiwa ni pamoja na kutuma taarifa za walipo, na kurekodi mawasiliano yao ya njia ya simu na mitandao ya kijamii.

Inasemekana kwa Uganda wafanyakazi wa kampuni hiyo walitoa msaada kwa vitengo vya kiusalama kuweza kufungua na kusoma meseji za kwenye simu ya mwanamuziki na mwanasiasa Bobi Wine.

INAYOHUSIANA  Udukuzi wa taarifa za wateja unatesa mabenki
Wafanyakazi wa Huawei wanahusika na udukuzi wa wanasiasa Afrika
Mwanamuziki na Mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine wa nchini Uganda

Wafanyakazi hao walifanikisha hayo kwenye ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi la nchini humo, walitumia programu ya udukuzi inayofanana kiutendaji na programu maarufu ya kampuni moja ya Israel, NSO Group, inayokwenda kwa jina la Pegasus spyware.

Msemaji wa Huawei amekana matukio hayo kufanyika.

Taarifa inakuja kipindi ambacho tayari serikali ya Marekani imekuwa ikijaribu kushauri washirika wake na mataifa mengine duniani kutotumia vifaa vya Huawei kwa madai ya vifaa hivyo kutokuwa salama dhidi ya udukuzi wa China.

Chanzo: WSJ na tovuti mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |