Tumeshaingia nusu yapili ya mwaka 2022 si vibaya tukatazama matoleo mapya ya simu za makampuni mbalimbali yanayotarajiwa kutoka katika kipindi hiki cha mwaka. Tutapangilia matoleo hayo kufuata mwezi ambao simu inategemewa kuzinduliwa, kuanzia hapa karibuni.
- Nothing Phone (1)
Kampuni ya Nothing imepanga kuzindua bidhaa yake ya pili, ikiwa ni Simu yao ya kwanza kabisa, ikiitwa Nothing Phone 1. Simu hii inaatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 12 mwezi huu, huku ikianza kuuzwa katika nchi ya India na bara la Ulaya.
Simu hii haitapatikana katika bara la Marekani kulingana na taarifa rasmi toka kampuni ya Nothing. Simu hio inatarajiwa kuja na chipset aina ya Qualcomm Snapdragon 778+ 5G, ikiashiria kwamba itakuwa ni simu yenye hadhi ya uwanda wa juu katika bajeti ya kati (High-end Midrange) na sio hadhi ya matoleo ya juu kabisa ya makampuni (Flagships)
2. Google Pixel 6a
Muendelezo wa matoleo ya kati kutoka kampuni ya Google unatarajiwa kuwa simu ya Google Pixel 6a, itakayozinduliwa rasmi mnamo Julai 28, mwaka huu. Simu hii inatarajiwa kuwa na ufanano na simu ya Google Pixel 6, huku wakibadilisha baadhi ya vifaa ili kupunguza gharama. Matoleo ya kati kutoka kampuni ya Google yamekuwa yakifanya vizuri hivyo tutarajie Pixel 6a kuwa simu nzuri na yenye ushawishi mkubwa katika kundi lake hasa kwa bei na sifa zake.
3. Samsung Galaxy Z Fold 4 na Z Flip 4
Matoleo rasmi ya nne ya simu za kukunja (Foldables) kutoka kampuni ya Samsung pia yanatarajiwa kuzinduliwa katika nusu hii ya mwaka. Simu za Galaxy Z Fold 4 na Z Flip 4 zinatarajiwa kuzinduliwa mwezi Agosti mwaka huu zikiwa na maboresho kutoka zile za mwaka jana.
Baadhi ya maboresho hayo yanatarajiwa kuwa ufanyaji kazi bora zaidi, kamera nzuri zaidi, ongezeko la betri kwa asilimia kadhaa, takribani asilimia tisa, mfumo mzuri zaidi wa kuzikunja pamoja na kioo bora zaidi. Kwa kuzingatia mafanikio ya matoleo yao mwaka jana, simu hizi zinatarajiwa kuendelea kukuza soko la simu za kukunja duniani kwa kuvutia watu wengi zaidi kuzinunua simu hizo.
- Apple iPhone 14
Toleo jipya la simu za Apple iPhone linnatarajiwa kutoka mwezi wa tisa mwaka huu, likiwa ni iPhone 14. Apple iPhone 14 inatarajiwa kuwa katika matoleo manne yakiwa ni iPhone 14, iPhone 14 Max, iPhone 14 Pro na iPhone 14 Pro Max. Simu hizi zinatarajiwa kuwa na maboresho makubwa sana hasa katika idara ya kamera pamoja na matumizi ya chaji, ambapo tayari iPhone 13 zimekwisha kufanya vizuri sana, simu hizi zinatoka zikilengwa kuboresha zaidi matumizi ya chaji katika simu za iPhone huku pia ufanyaji kazi wa kamera ukipata maboresho zaidi, mojawapo ikiwa kuongezwa kwa ukubwa wa sensa katika simu za Pro, kutoka MegaPixel 12 hadi Megapixel 48.
- Google Pixel 7 na 7 Pro
Simu hizi ambazo ndizo toleo kuu lijalo kwa kampuni ya Google zinatarajiwa kutoka mnamo mwezi wa kumi mwaka huu. Japokuwa mwezi wa kumi yaweza kuonekana bado ni mbali kidogo, kampuni ya Google ilikwisha kuweka wazi simu hizo kwa umma tangu mwezi wa tano mwaka huu, ikionesha mabadiliko kidogo katika muundo wake wa nje ilioutambulisha kuanzia simu za Pixel 6, na pia zikitarajiwa kuja na chipset mpya ya Google Tensor 2 ambayo ni ya Google binafsi, ikitarajiwa kuleta maboresho katika ufanyaji kazi wa simu kwa ujumla.
Hizi si simu pekee zinazotarajiwa kuzinduliwa katika kipindi hiki cha mwaka, baadhii ya nyingine zikiwa
–Â Xiaomi 12S Ultra
– ASUS ROG Phone 6
– Huawei P60
– Motorola Frontier
– Nokia 10 Pureview
– Google Pixel Fold
– HTC Desire 22
Orodha yaweza kuendelea zaidi, ila haya ni kwa ufupi, yale ambayo yanatarajiwa kwa shauku kubwa na wapenzi na watumiaji wa simu kote duniani. Taarifa zaidi kuhusu kila mojawapo zitaendelea kukujia kupitia hapa hapa kwenye kona ya Teknolojia.
No Comment! Be the first one.