Imefahamika toleo la Google Play Store 18.3.82 linasababisha kuisha kwa chaji kwenye simu za Android haraka kuliko kawaida.
Toleo hilo ambalo limetoka hivi karibuni limeonekana kuwa na tatizo (bug) linalosababisha utendaji wake kutumia chaji nyingi ya simu.
Kama una muda mrefu haujasasisha(update) toleo la app ya Google Playstore basi usiwe na wasiwasi ila kwa watu waliofanya hivyo hivi karibuni basi wanaweza wakawa nao wameathirika na hili.
Kwa baadhi ya watumiaji walikuta Google Playstore ikila zaidi ya asilimia 20% ya matumizi ya chaji kwenye simu zao. Kujua kama umeathirika fika kwenye mipangilio (settings) eneo la betri na kuangalia app gani zinakula asilimia kubwa ya chaji ya simu yako. Kama app ya Google PlayStore inatumia sana chaji na wakati hauitumii basi inawezakana ukawa umeathirika na tatizo hilo.
Toleo hili la Google Play Store limetoka hivi karibuni na tayari Google wamekubali kuonekana kwa tatizo hilo na wanalifanyia kazi kuhakikisha kuna toleo jipya mapema iwezekanavyo.
Kutatua;
- Njia ya 1: Nenda eneo la masasisho (updates) na angalia kama kuna toleo jipya na kubali kusasisha Play Services.
- Njia ya 2: Njia nyingine ni kudownload toleo la nyuma la Play Services, ubaya hapa ni kwamba bado app inaweza ikajisasisha
- Njia ya 3: Kujiunga katika toleo la beta kwa muda, unaweza kujiunga toleo la Google Play Store Beta hapa -> Google Play Beta (Toleo la beta linaweza likawa na matatizo madogo madogo)
Pia unaweza kudownload toleo la beta hapa -> APK (Google Play Store)
Baadhi ya malalamiko ya watu mtandaoni:
Here we go again with the secret battery assassin Google Play services that updates in the background and stabs your phone right in the heart. pic.twitter.com/Zu8jRchzYq
— Artem Russakovskii (@ArtemR) August 9, 2019