fbpx
apps, Intaneti, whatsapp

WhatsApp Business yaanza kupatikana; Sasa unaweza ukafungua akaunti ya kibiashara

whatsapp-business-yaanza-kupatikana-kwa-makampuni-wafanyabiashara
Sambaza

Baada ya kipindi kama cha mwezi mmoja WahatsApp ilitangaza kuja na mpango wa kufungua akaunti za kibiashara kwa watumiaji wake sasa tayari wamefungua akaunti hiyo itakayojulikana kama WhatsApp Business.

Kwa ujio wa WhatsApp Business kutasaidia sana wafanyabiashara au kampuni kutenganisha mazungumzo binafsi na yanayohusu biashara na tayari WhatsApp Business tayari inapatikana Play Store kwa watumiaji wa toleo la Beta na ipo katika kipindi cha majaribio ili kupokea maoni ya watumiaji na kurekebisha penye mapungufu.

Uzuri wa WhatsApp Businees unaweza kupanga muda wa kupokea sms kitu ambacho  kitapunguza kero kwa kuingia meseji hata usiku wa manane kama ilivyo kwa WhatsApp ya kawaida.

Kalenda ya kwenye WhatsApp itakayokuwezesha kupangilioa mpango kazi wa biashara yako.

Pia kutakuwa na mipangilio mbalimbali kulingana na biashara yako. Aidha utakuwa unaona idadi ya meseji ulizotumiwa na zile ulizotuma ili kuona muitiko wa wateja wako kwa biashara yako na kufanya tathmini.

INAYOHUSIANA  Kiswahili kuwa lugha ya kwanza Afrika kutambuliwa Twitter
Unaweza kutumia WhatsApp Business na WhatsApp ya kawaida kwenye simu moja lakini ziwe na namba tofauti.

Unaweza kuweka picha yako au logo ya kampuni yako ili iwe rahisi kutambulika na wateja wako au wale unaoshirikiana nao katika mambo ya biashara. Inawezesha kuweka mpangilio wa maelezo ya kampuni/biashara yako kama tovuti, anwani/barua pepe na hata kuweka ujumbe maalumu utakaokuwa unajibu wateja wako bila ya wewe kuwepo hewani.

Baada ya kufungua akaunti ya WhatsApp Business kitakachofuata ni kupata utambulisho rasmi (Verified Accounts) kama ilivyo kwa Facebook, Twitter na Instagram.

Logo ya WhatsApp Business imebaki ileile kama ya Whatsapp ya kawaida lakini ina mabadiliko kidogo ambapo katikati kuna herufi B, ili kueleta utofauti na ile ya kawaida.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.