fbpx

Huawei, simu

Huawei: Programu Endeshaji ya Harmony OS itakuwa tayari kwa ajili ya simu Disemba hii

huawei-programu-endeshaji-ya-harmony-os-itakuwa-tayari

Sambaza

Huawei wamekuwa kazini kwa miezi kadhaa wakitengeneza programu endeshaji ya ziada dhidi ya Android. Na sasa ni rasmi programu endeshaji ya Harmony OS itakuwa tayari kwa ajili ya kutumika kwenye simu kufikia Disemba mwaka huu.

Huawei wamesema toleo la kiwango cha beta litakuwa tayari kwa watengenezaji simu za mkononi (beta ni kiwango cha ubora unaoweza kutumika bila kuleta shida).

Rais wa masuala ya teknolojia katika upande wa Huawei unaohusika na biashara za bidhaa amesema kufikia Januari au Februari mwakani tayari tutegemee kuona simu zinazotumia programu endeshaji hiyo.

 Harmony OS itakuwa tayari
Inategemewa programu endeshi ya Harmony OS itakuwa tayari kwa makampuni ya utengenezaji simu pamoja na watengeneza apps kufikia Disemba 2020

 

Ingawa mabadiliko ya kiongozi wa serikali ya Marekani kutoka kwa Bwana Trump, kwenda kwa Rais aliyeshinda uchaguzi kwa sasa Bwana Joe Buden yanaweza kuleta mabadiliko flani katika katazo la kibiashara dhidi ya Huawei lakini Huawei bado hawategemei mabadiliko makubwa sana.

INAYOHUSIANA  Huawei P9, Simu inayovutia yenye skendo ya Kuiga Ubunifu wa iPhone! #Uchambuzi

Programu endeshi ya Harmony OS inategemea kuweza kuleta ushindani dhidi ya programu endeshaji ya Android. Huawei iliwalazimu kuja programu endeshaji yao ili kujiokoa kutoka kwenye vikwazo vya Marekani vinavyowabana kuweza kufanya kazi na Google, ambao ndio wamiliki na walezi wa programu endeshaji ya Android.

Je una mtazamo gani na maendeleo haya kutoka Huawei? Je unadhani watafanikiwa?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*