fbpx

simu, Tecno, Uchambuzi

Tecno Camon 16s ipo Njiani Kuingia Sokoni Hivi Karibuni

tecno-camon-16s-ipo-njiani-kuingia-sokoni

Sambaza

Simu ya Tecno Camon 16s ipo njiani kuingia sokoni. Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO inatarajia kuzindua simu mpya ya TECNO CAMON 16s muda wowote kuanzia sasa.

Camon 16s ni simu ambayo inakuja na teknolojia kubwa ya kamera na uwezo mkubwa  utakaowanufaisha watumiaji katika shughuli zao za kiofisi na kiuchumi.

Taarifa kutoka kampuni ya TECNO zinaeleza kuwa TECNO CAMON 16s ina kamera nne nyuma na kamera kuu ikiwa na 48MP.

INAYOHUSIANA  Simu janja 7 kutoka China ambazo hazijulikani na wengi! (2017) #Uchambuzi

Kamera hiyo yenye uwezo wa kuchukua picha ang’avu bila kujalisha mazingira au muda ambao picha inapigwa hata kwenye mwanga hafifu simu hiyo ina uwezo wa kupiga picha ang’avu kutokana na flashi zake nne za nyuma pamoja na lensi yenye teknolojia ya AI ambapo vyote kwa pamoja vinamsaidia mtumiaji wa simu hii kupata picha ang’avu hata kwenye mazingira yenye mwanga hafifu.

INAYOHUSIANA  Xiaomi wazindua simu mbili zenye kamera ya selfie yenye megapixel 16
tecno camon 16s ipo njiani
Tecno Camon 16s Ipo Njiani: Muonekano wake wa mbele na nyuma

Pamoja na kuwa na kamera kubwa yenye uwezo, pia simu hiyo imedokezewa kuwa ina memori kubwa inayofikia GB 128 ROM kwa GB 4 RAM. Ukubwa wa memori ya simu hii utamsaidia mtumiaji kuhifadhi vitu vyake bila kufuta pia kuiwezesha simu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kukwama.

Vilevile simu hiyo ya TECNO CAMON 16s ina Skrini kubwa ya inchi 6.6 itakayompa mtumiaji furaha na uhuru wa kutazama video, kucheza gemu pamoja na kupiga picha zinazojitosheleza na kuenea vizuri kwenye screen ambazo zitakuwa zinaleta uhalisia wa picha halisi.

INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy na simu za toleo la M20 na M30

camon 16s ipo njiani
Inakuja na skrini ya ukubwa wa inchi 6.6

Kufahamu zaidi ujio wa simu hii bofya link kwenda kwenye ukurasa wao wa Instagram;

https://cutt.ly/VgDoVDQ

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*