fbpx
Airtel, Barua pepe, BIS, Blackberry, Intaneti, simu, Tanzania

Airtel: Wapanga Gharama Raisi Zaidi Kwa Ajili ya Blackberry!

Sambaza

Kampuni ya mawasiliano ya Airtel imeleta mfumo wa malipo raisi zaidi kwa ajili ya makundi tofauti ya wateja.

Nilichopenda katika mfumo huu ni kuwa wamegundua aina ya wateja walionao na wamekuja na mfumo wa malipo wa makundi matatu, ambayo kwa kifupi naweza sema ni mfumo wa malipo utakaweza kutumiwa na makundi muhimu kama vijana na wafanyakazi ‘in terms of affordability’.

BIS -30,000/= kwa mwezi, KAMILI – 17,500/= kwa mwezi, 5,000/= kwa wiki na 1,000/= kwa siku, GENGE- 12,000/= kwa mwezi, 3,500/= kwa wiki na 700/= tu kwa siku.

Chaguo la kwanza la BIS linampatia mteja wa AIRTEL huduma zote za Blackberry, la pili ni ‘KAMILi’ ambalo utaweza kuunganisha akaunti moja tuu ya barua pepe. Hivyo kwa wale wanaotumia simu za Blackberry kwa ajili ya kupata huduma za barua pepe kutoka kwenye akaunti mbalimbali itakulaxima kutumia huduma ya BIS kwa bei ya 30,000/=.
Kwa huduma ya GENGE vitu muhimu utakavyokosa ni pamoja na huduma zote za barua pepe, pamoja na huduma za kuchat za jamii ya google, yahoo na hotmail messenger, lakini ile BBM itakuwa inapatikana. Na katika zote, GENGE na KAMILI, huduma ya BLackberry Protect inayokuwezesha kufanya ‘back ups’ ya data zako muhimu itakosekana, itapatikana kwa wale wa BIS tuu.

Unaonaje hili? Nimefuraishwa sana na mgawanyiko huu wa bei, kwani umeweza kuona maitaji tofauti ya wateja wake na naamini washindani wasipofanya mabadiliko kama haya basi muda si mrefu tutaona wengi zaidi wakitumia Airtel kwa huduma za Blackberry, kumbuka wengi wetu tuna simu zaidi ya moja hivyo kubadilisha laini na simu haitakuwa tatizo.
Kuna kitu nimeona katika ukurasa wa Facebook wa Zantel kama nao wamefanya mgawanyiko kama huu kwa huduma za Blackberry lakini sijafanikiwa kuona maelezo yeyote popote. Nitajitahidi kuwasiliana nao nione kunani…
Endelea kusoma Teknokona!
Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Simu Janja 5 Zinazosubiriwa Kwa Hamu!
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*