Kama unafuatilia mara kwa mara mtandao wako namba moja kwa habari za kiteknolojia katika lugha maarufu ya Kiswahili basi utakuwa unafahamu ya kwamba mwezi huu ndio toleo jipya la programu endeshaji la Windows linakuja. Yaani Windows 10.
Ilikuwa inategemewa kufikia tarehe 29 mwezi huu kila mtu mwenye nakala halali ya Windows 7 aweze kupakua programu endeshaji ya Windows bure kabisa wakati wengine wakiwa na uwezo wa kulilipia mtandaoni kabla ya kusubiri kulipata katika diski za USB (Flash Disk). Lakini katika uamuzi ambao wengi wanaona ni uamuzi usio mzuri kwa kampuni ya Microsoft wamesema ya kwamba toleo hilo halitapatikana kwa wakati mmoja kwa watu wote.
Soma pia – Windows 10 Kuuzwa katika USB – Flash Disks
Kama unatumia kompyuta inayotumia toleo halali la Windows 7 basi kampuni hiyo itakuwa inaruhusu upakuaji wa toleo la Windows 10 kwa hawamu hawamu. Na haijafahamika hawamu hizi zitakuwa ni za muda gani.
“Inategemewa kupitia programu yao ya kusasisha Windows, yaani ‘Windows Update’ wataweza kukupa taarifa pale ambapo toleo hili la Windows 10 lipo tayari kushushwa na kupakuliwa katika kompyuta yako”
Sababu kuu waliyoitoa ni kwamba wanataka kuhakikisha toleo hilo linaingia katika ubora wake katika kompyuta zote zenye haki na sifa ya kupata toleo hilo kupitia njia ya mtandao.
Wengi wameona hatua hii haina uzuri wowote lakini ni jambo la kufahamu ya kwamba hii ni mara ya kwanza kampuni hii inajaribu mfumo wa kusasisha (update) mfumo mzima wa programu endeshaji ya Windows kwa kutumia intaneti (kupitia programu ya Windows Update).
Soma Pia – Windows 10 Bure Kwa Wengi Ila Itakuwa Tsh Laki 2 Kwa Wengine
Je ulikuwa nawe unasubiria kwa hamu kusasisha programu endeshaji ya Windows katika kompyuta yako? Endelea kusubiri.
No Comment! Be the first one.