fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
simu

Hii Ndio Simu ya Kwanza ya BlackBerry Inayotumia Android?

Hii Ndio Simu ya Kwanza ya BlackBerry Inayotumia Android?

Spread the love

Mapema mwezi wa sita tuliandika kuhusu uamuzi wa kampuni maarufu ya BlackBerry kuleta simu zinazotumia Android sokoni. Uamuzi huu kwa wengi ulipokelewa vizuri kwani tayari ingawa kampuni imeshatoa simu nyingi zenye mvuto katika miaka ya hivi karibuni hazikufanikiwa sana sokoni kwa sababu tayari watumiaji wengi wanataka programu endeshaji iliyoshiba katika eneo la apps mfano wa Android na iOS.

Simu hiyo ishawahi kuoneshwa katika mkutanao mmoja wa BlackBerry lakini ilikuwa bado haifahamiki kama itakuja na toleo la Android

Simu hiyo ishawahi kuoneshwa katika mkutanao mmoja wa BlackBerry lakini ilikuwa bado haifahamiki kama itakuja na toleo la Android

Picha za inayoonekana kuwa ni simu kutoka BlackBerry ikiwa inatumia toleo la programu endeshaji ya Android imesambaa mtandaoni kuanzia jana. Simu hiyo yenye eneo la kibodi (keyboard) imeanza kusambazwa na mtu mmoja maarufu katika kutoa taarifa za uhakika za kisiri kuhusu makampuni mbalimbali ya elektroniki hasa hasa kwenye masuala ya simu.

BlackBerry Venice

BlackBerry Venice

Je itakuja lini?

Simu hiyo inayofahamika kwa jana la BlackBerry Venice inategemewa kuingia sokoni ikifika mwishoni mwa mwaka huu na bei pia bado haijajulikana.

[socialpoll id=”2276589″]

Wengi wanategemea simu hiyo kufanikiwa kwani katika simu janja nyingi zilizopo sokoni kwa sasa bado hakuna simu tamu yenye kibodi, na hivyo inategemewa wengi ambao bado walikuwa na mapenzi ya simu kutoka BlackBerry watapata sababu nzuri ya kurudia kununua simu za kampuni hiyo.

SOMA PIA  Vodacom Tanzania yazindua mfumo wa mawasiliano wenye kasi ya 5G nchini.

Soma – Blackberry Kutoa Toleo La Simu Itakayotumia Android!?

Endelea kutembelea mtandao wa TeknoKona na tutakutaarifu zaidi kuhusu ujio wa simu hii habari zikizidi kutufikia.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania