fbpx
Android, apps, Google

Google wanakuja na Fastshare, watumiaji wa Android kuweza kutumiana mafaili kwa kasi zaidi

google-wanakuja-na-fastshare
Sambaza

Google wanakuja na teknolojia ya Fastshare ambayo itapatikana katika toleo lijalo la Android ambalo linaenda kwa jina la Android Q kwa sasa – jina kamili hutambulishwa mbeleni.

Mtumiaji wa Android wataweza kutuma na kupokea mafaili makubwa kutoka kwa mtumiaji mwingine kwa kasi zaidi.

Kwa muda mrefu kwenye Android teknolojia ya kuhamisha mafaili kutoka simu moja hadi nyingine imekuwa ni teknolojia ya Android Beam. Teknolojia ya Android Beam imekuwa ikitegemea kifaa cha teknolojia ya NFC – ambayo ilikuwa inawezesha kutuma mafaili kutoka simu moja hadi nyingine ila kwa KASI NDOGO.

INAYOHUSIANA  BlackBerry Messenger (BBM) kufungwa Mei 31

Teknolojia mpya ya Fastshare itakuja ikiwa inategemea teknolojia ya Bluetooth pamoja na teknolojia ya WiFi ambayo ipo kwenye simu janja zote kwa sasa. Kwa kutumia teknolojia ya WiFi mafaili yataweza kutumwa kwa kasi zaidi.

fastshare

Kwa muda mrefu tayari Apple alileta teknolojia ya namna hii kwa vifaa vyake vya iOS na MacOS – ikitambulika kwa jina la AirDrop. Mtumiaji mmoja wa kifaa cha Apple anaweza kutuma faili kubwa kwenda kifaa kingine ndani ya sekunde hadi dakika chache.

INAYOHUSIANA  Amazon kuunda programu ya kujipima nguo

Inavyofanya kazi;

  • Kwa kutumia teknolojia ya Bluetooth – vifaa viwili vinatengeneza mawasiliano na kuandaa teknolojia ya WiFi kutumika
    Kisha kwa kutumia teknolojia ya WiFi mafaili yanatumwa kutoka kifaa kimoja kwenda kingine
  • Kumbuka haitumii huduma ya intaneti ya kawaida, haya ni mawasiliano ya moja kwa moja kutoka kifaa kimoja kwenye kingine.

Uzuri wa FastShare kutoka Android ni kwamba watumiaji wataweza kutuma mafaili hadi kwa vifaa vya Apple, wakati kwa AirDrop mawasiliano ni kati ya vifaa vya Apple tuu.

INAYOHUSIANA  Picha mnato kwenye IG zinaboreshwa
android fastshare
Kwa kutumia teknolojia hii watumiaji wa Android wataweza kuwatumia mafaili hadi watumiaji wa vifaa vya Apple

Toleo lijalo la Android linalobeba jina la siri la Android Q kwa sasa linategemewa kutambulishwa mwezi wa nane mwaka huu. Baada ya hapo ndio taarifa kuhusu upatikanaji wa teknolojia hiyo kwenye matoleo mengine yaliyopita ya Android itawekwa wazi.

Vyanzo: XDA na vyanzo mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |