fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps whatsapp

WhatsApp haitafanya kazi 2021 katika Simu Hizi za Android na iPhone

WhatsApp haitafanya kazi 2021 katika Simu Hizi za Android na iPhone

WhatsApp haitafanya kazi 2021 katika simu kadhaa zinazotumia Android na iOS. Sababu zikiwa ni za kiusalama na za kiteknolojia.

Ni kawaida kila baada ya miaka kadhaa kwa WhatsApp kuacha kufanya kazi au kutotolewa kwa matoleo mapya/masasisho kwa baadhi ya simu.

Mara nyingi sababu kuu huu ni simu hizo kufikia mwisho wa kupokea masasisho (updates) ya programu endeshaji (os).

WhatsApp haitafanya kazi 2021

WhatsApp haitafanya kazi mwaka 2021 kwenye simu mbalimbali – za Android na iOS

WhatsApp ni moja ya app maarufu duniani na moja ya app muhimu kwa watumiaji wa simu janja za aina zote, iwe Android au za iPhone.

Kwa iPhones

Simu za iPhone zinazotumia programu endeshaji ya iOS ya chini ya toleo la 9 (iOS 9) zote zitakosa kupata app ya WhatsApp tena. Kwa sasa hii ina maanisha simu za iPhone 4 na nyingine zote zilizotoka kabla yake.

SOMA PIA  Instagram yaleta Chaneli kwa ajili ya Video za matamasha

Kwa watumiaji wa simu za 4S, 5, 5S, 5C, 6 na 6S watatakiwa kuhakikisha wanatumia toleo la iOS 9 au jipya zaidi ili kuweza kuendelea kutumia app hii maarufu ya mawasiliano.

Kwa simu za Android

Kama simu unayotumia ina toleo la Android la 4.0.2 na nyuma basi itakuwa ndio mwisho wa kuweza kutumia app ya WhatsApp. Simu ambazo hazina uwezo wa kupata toleo la Android la juu zaidi ya hapo ni pamoja na HTC Desire, Motorola Droid Razr, na Samsung Galaxy S2. Simu hizi hazitakuwa na uwezo tena wa kutumia app ya WhatsApp.

SOMA PIA  Firefox Sasa Kupatikana Apple store Kwa Watumiaji wa iPad na iPhone

Je utahakikishaje kama simu yako ipo salama?

Hakikisha simu yako inatumia toleo la kisasa la programu endeshaji (OS).

Jinsi ya kuangalia toleo la programu endeshaji la simu yako.

iPhone:

Bofya Settings > General > Information

Hapo utaona kuhusu taarifa za toleo la programu endeshaji yako.

SOMA PIA  Apps Za Mahusiano Zahusishwa na Ongezeko la Maambukizi ya Magonjwa ya Ngono

Android:

Bofya Settings > About System/Device

Hapo utaona taarifa kuhusu toleo la programu endeshaji yako.

Soma makala na maujanja ya WhatsApp -> Teknokona/WhatsApp

Kama utaona toleo unalotumia kwenye simu yako ni kati ya matoleo tuliyoyataja kwamba hayatakuwa na uwezo wa kutumia app ya WhatsApp tena basi hakikisha unasasisha/update.

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. My phone tekno fg lite Android 8.0 je itafungiwa kutumia watsaap?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania