fbpx
Huawei, simu, Teknolojia

Huawei Mate 20X ya 5G yaingia sokoni

huawei-mate-20x-ya-5g-yaingia-sokoni
Sambaza

Dunia nzima inafahamu vuta nikuvute/vikwazo ambavyo Huawei Technologies imekuwa ikikumbana navyo kwa miezi kadhaa kitu ambacho kimechelewesha kuingia sokoni kwa bidhaa mbalimbali hasa zinazotumia 5G.

Tulishaandika mara kadha kuhusu Huawei na simu janja zenye teknolojia ya 5G ingawa zilikuwa bado hazijaingia sokoni mpaka kumi la pili kwa mwezi Julai; Huawei Mate 20X yenye 5G ilitakiwa kuzinduliwa mwezi Juni huko Uingereza lakini kutokana na sababu mbalimbali hilo halikuwezekana. Hata hivyo, inaonekana mambo yameanza kuinyookea kampuni husika kwani simu hiyo imeingia sokoni UK na Umoja wa falme za Kiarabu (UAE).

INAYOHUSIANA  Instagram Lite imerudi na toleo jipya

Je, sifa zake ni zipi?

Huawei Mate 20X (5G) ni simu ambayo bado uzinduzi wake haujafanyika ingawa tayari sifa muhimu zimeshafahamika:

Kipuri mamaBalong 5000 (ndio inayowezesha teknolojia ya 5G kwenye simu husika)

Urefu wa kioo: inchi 7.2 (OLED)

Memori: RAM-GB 8, diski uhifadhi-GB 256

Kamera: Nyuma zipo 3-MP 40, MP 20 na MP 8. Mbele ipo moja-MP 24

INAYOHUSIANA  TTCL yawapa serikali gawio la Tsh 1.5 bilioni

Betri: 4200mAh na teknolojia ya kuchaji haraka kiwango cha 40W

Mtandao+Programu endeshi: GSM / HSPA / LTE / 5G. Itakuwa inatumia Android 9

Huawei Mate 20X
Huawei Mate 20X (5G) ambayo pia inatumia kalamu janja.

Mpaka sasa rununu (simu janja) husika imeingia sokoni kwenye nchi za Falme za Kiarabu kwa $960|Tsh. 2,246,400. Kiujumla simu husika itazinduliwa Julai 22 2019, Julai 26 itazinduliwa nchini Uchina na itauzwa $1,240|Tsh. 2,901,600.

Vyanzo: Huawei, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|