fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple

Fahamu Mambo Mapya ktk iOS 9; Pia Fahamu Jinsi ya Kupakia kwenye iPhone au iPad

Fahamu Mambo Mapya ktk iOS 9; Pia Fahamu Jinsi ya Kupakia kwenye iPhone au iPad

Spread the love

Mapema Jumatano hii, Apple wameachia mfumo wa 9 wa kuongoza simu na tabiti zake unaojulikana kama iOS9, na kuruhusu mamia kwa maelfu ya watumiaji wakiwa makini kushusha mfumo huo mpya, unaotazamiwa kufanya vizuri sokoni kutokana na kujaa mambo mapya yanayovutia watumiaji wake.

Apple wameachia mfumo wa iOS 9 kuunga mkono vifaa vyake vipya kama iPhone 6S, TV ya Apple pamoja na iPad Pro vilivyozinduliwa mjini San Fransco mapema mwezi huu.

Aina ya iPhones na iPad zitakazoweza kutumia iOS 9

Aina ya iPhones na iPad zitakazoweza kutumia iOS 9

Miongoni mwa vifaa vitakavyokua vinaingiliana na iOS 9 ni pamoja na iPhone 6S, iPhone 6S Plus, iPhone 6, iPhone 6 Plus, iPhone 5s, iPhone 5c, iPhone 5 na iPhone 4s, iPad Air 2, iPad Air, iPad 4, iPad 3 na iPad 2, iPad mini 3, Retina iPad mini, iPad mini toleo la 1, iPod touch toleo la 6, iPod touch toleo la 5.

IOS 9 inatazamiwa kupakuliwa kwa kasi kwa simu janja za iPhone pamoja na iPad kutokana na maboresho na vitu vingine mbalimbali vitakavyowezeshwa kwa mara ya kwanza kwa watumiaji wa iOS. Tutakudokeza baadhi ya sifa zake mpya na za muhimu zaidi katika toleo hili jipya la programu endeshaji maarufu ya iOS.

NAMNA MPYA YA KUVUTIA YA KUPATA HABARI

App ya Apple News itakuletea habari mbalimbali kwa haraka zaidi

App ya Apple News itakuletea habari mbalimbali kwa haraka zaidi

iOS 9 wanakuletea app mpya katika simu yako itakayokua inakuletea habari zote ambazo huwa unavutiwa nazo. Hutakuwa na haja ya kuzunguka katika mitandao au magazeti kutafuta habari, badala yake iOS9 inakuletea katika kioo cha simu yako wakati utakao. Utachagua aina ya habari unazotaka, kutoka katika chanzo cha habari unachokiamini, na iOS9 itakuletea kwenye simu yako.

SOMA PIA  Mapya kutoka Apple: MacBook Air 2018 na Mac Mini mpya

SIRI SASA KUWA NA AKILI ZAIDI NA MARADUFU.

SIRI sasa imeongezwa uwezo wa kufikiri na kujibu maswali mengi na kwa ufasaha zaidi hivyo kumsaidia sana mtumiaji wake.

SIRI sasa imeongezwa uwezo wa kufikiri na kujibu maswali mengi na kwa ufasaha zaidi hivyo kumsaidia sana mtumiaji wake.

Wakati iOS8 walipokuja na SIRI, matumizi yake yalikuwa yamebanwa kwa baadhi ya huduma tu, na wakati mwingine kushindwa kufanya baadhi ya vitu. Sasa iOS9 wanakuja na namna mpya katika SIRI inayojulikana kama SIRI Proactive. Sasa SIRI ataweza kutafuta machaguo mengi zaidi na kujibu hata maswali mengi zaidi atakayoulizwa.  SIRI atatoa majibu mengi na baadhi hata kabla hajaulizwa, atakuwa na uwezo wa kupendekeza matumizi kwa mtumiaji wake.

TUMIA IPAD YAKO NA HUDUMA MPYA YA ‘MULTITASKING’.

Uwezo wa kutumia apps mbili kwa wakati mmoja unakuja rasmi

Uwezo wa kutumia apps mbili kwa wakati mmoja unakuja rasmi

Uwezo wa kutumia app mbili kwa wakati mmoja umekua ni ndoto kwa watumiaji wengi wa iPad. Lakini sasa, iOS9 wanafanya ndoto hizo kuwa kweli. Sasa watumiaji wake wataweza kuwasha app mbili kwa wakati mmoja, kutelezesha app moja kufungua nyingine, kutazama picha mbili kwa wakati mmoja kwa kugawanya kioo. iOS9 ni Bomba.

MATUMIZI MAPYA NA MAZURI ZAIDI YA BETRI YA KIFAA CHAKO.

SOMA PIA  Asilimia Ya chaji Katika iPhone Kurudi Sehemu Yake Zoeleka!

Wakati Apple walipozindua iOS 8, watumiaji wengi walilalamika kukaukiwa na chaji za vifaa vyao, na hata baada ya marekebisho kufanyika katika matoleo yaliyofuata, bado matokeo hayakuridhisha. Sasa, iOS 9  wameanzisha Mode ya kuhifadhi nguvu ya betri yako kwa mara ya kwanza katika vifaa vya Aple (Power Save Mode).

Uwezo wa betri ya kifaa chako umeboreshwa mara dufu kupitia iOS9

Uwezo wa betri ya kifaa chako umeboreshwa mara dufu kupitia iOS9

Sasa kuna uwezo mpya kwa kutumia chaji ya kifaa chako, kwa kutumia mfumo mpya wa matumizi ya app zako ulioandaliwa na Apple. Apple wamepunguza matumizi ya nguvu nyingi katika app na kufanya kutumia nguvu ndogo ya umeme hivyo kuongeza maisha zaidi ya betri yako. Sasa Apple wamehakikishia wateja wao uhakika wa zaidi ya saa moja la ziada kutoka katika iOS 9 kabla ya kuchaji betri zao.

MATUMIZI MAPYA YA UANDISHI WA NOTES ZAKO

iOS9 inakuletea app ya notes iliyoboreshwa zaidi, na vipengele vilivyotanuliwa zaidi ikilinganishwa na iliyokuwepo mwanzoni. Sasa  mtumiaji ataweza kuchagua namna ya maandishi ya maneno yake, na hata kuchorea michoro kama sehemu ya kumbukumbu zake. Mfano, unaandaa kumbukumbu kwa ajili ya nyumba yako mpya unayoijenga. Utaweza kuandika bei ya vifaa mbalimbali, vipimo kwa maandishi tofauti, na hata michoro ya vifaa ivyo kisha kuhifadhi kwa matumizi ya baadae.

mpangilio mpya wa uandishi wa notes zako

mpangilio mpya wa uandishi wa notes zako

Japo kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya watumiaji wa vifaa vya Apple kushindwa kushusha na kuhifadhi mifumo hii, inashauriwa kuwa na subira kwani hilo linaweza kusababishwa na msongamano mkubwa wa watumiaji katika mtandao wa Apple kila mmoja akitaka kushusha mfumo huu. Kama muda ukifika, hali itakua shwari, na utaweza kufurahia maisha mapya ya kifaa chako. iOS 9 ni Bomba.

SOMA PIA  Apple na Oprah kufanya kazi kwa pamoja

JINSI YA KUSHUSHA NA KUHIFADHI IOS9 KWA KUTUMIA iTUNES

Kabla ya kushusha na kuhifadhi mfumo huu, unashauriwa kufata hatua zifuatazo,
1. Tengeneza ‘Backup’ ya kifaa chako kwenye kompyuta au iCloud
2. Hakikisha una toleo la karibu zaidi la iTunes
3. Chomeka kifaa chako kwenye kompyuta kwa kutumia waya mzuri wa kifaa chako, na subiri iTunes ikiunganishe.
4. Bonyeza kitufe cha kifaa chako kilicho juu upande wa kushoto wa iTunes yako.
5. Bonyeza kitufe kilichoandikwa ‘Check for Updates’ katika iTunes. Kama updates za kifaa chako ziko tayari, iTunes inashusha na kuhifadhi mfumo wenyewe katika kifaa chako 6. Utapokea ujumbe kutoka katika simu na iTunes kuwa, iTunes sasa inashusha na kuhifandhi mfumo mpya katika kifaa chako. Kubali kwa kubonyeza kitufe cha ‘Agree’na endelea kuanza zoezi.
7. iTunes sasa itashusha na kuanza kuhifadhi mfumo wa iOS 9 katika kifaa chako. Itatumia muda kidogo katika kushusha kwani itashusha hadi ukubwa wa 2GB, inategemea na kasi ya internet yako.
8. Kifaa chako kitazima na kuwaka mara mbili, usihofu. Cha msingi kamwe usichomoe kifaa chako.
9. Ikimaliza, utaona ujumbe wa ‘Hello’. Fata maelekeza ya kwenye kioo chako kumalizia kuhifadhi mfumo mpya.

Pia unaweza kusasisha (update) iPhone au iPad yako bila kutumia iTunes kwa kuenda sehemu ya Settings, kisha General alafu Sotware Update. Hakikisha kifaa chako kina intaneti ya uhakika.

Je ni jambo gani umefurahishwa nalo zaidi katika iOS 9? Fahamu kuhusu iPhone 6S na 6S Plus kwa kubofya HAPA!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania