Snapchat ni mtandao wa kijamii unaohusisha kutumiana ujumbe, picha na video ambavyo unaweza kuviona mara moja tuu na si vinginevyo. Mpaka sasa snapchat inaruhusu kutazama tena meseji uliyotumiwa (kwa mara ya pili) mara moja kwa siku na hiyo ni kama iliwahi kufutika na ulikua hujaisoma vizuri.
Snapchat wametangaza kuwa itakuwa inawachaji watumiaji wake senti 99 za kimarekani ili watazame video (meseji) ambazo zimefutika upya (Kwa mara nyingine). Zoezi hili linaonyesha kuwa Snapchat wamejiingiza katika rasmi katika kutengeneza pesa kupitia watumiji wake. Endapo ukilipia senti hizo basi utapata kuangalia ulichokua unataka (video, picha) bila shaka kwa unaweza rudia kuangalia hadi mara tatu (3) tuu.
Senti 99 ni sawa na dola 0.99 za kimarekani ambayo pia mara nyingi inachukuliwa kama ni dola moja tuu. Wakati WhatsApp wanakuchaji dola 0.99 za kimarekani kwa mwaka Snapchat wanakuchaji kuangalia tena meseji uliyoipata kwa gharama hiyo hiyo. Kwa haraka haraka kwa sasa senti 99 ni sawa na shilingi 2,152.02 za kitanzania (kwa makadirio)
Kwa sasa Snapchat ina watumiaji milioni 100, endapo watumiaji wake wakianza kulipa dolla za kimarekani 0.99 ili kuangalia meseji zao kwa mara nyingine tena kampuni itajipatia mapato makubwa. Kumbuka kampuni mpaka sasa lina thamani ya dola bilioni 19 za kimarekani. Bado muda mchache tuu thamani yao ipande pindi watakapoanza kuingiza hela hizo.
Licha ya hivyo hii sio njia pekee ya snapchat kuingiza hela. Kumbuka wana kipengele cha ‘Discover’ katika App yao ambacho kinaonyesha matangazo mbali mbali. Mtumiaji wa App hiyo halazimishwi kutazama matangazo hayo kwani ni hiari yake mwenye kama atazame au asitazame.
No Comment! Be the first one.