fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti Uchambuzi

Kurasa Zinazoongoza Kuhaririwa Katika Wikipedia!

Kurasa Zinazoongoza Kuhaririwa Katika Wikipedia!

Spread the love

Wikipedia ni sehemu ambayo mtu yeyote anaweza kujiandikisha na kisha kuandika kitu/vitu kuhusu topiki fulani. www.wikipedia.org inatumia mfumo wa wiki —Yaani mtu yeyote anaweza andika kitu katika mitandao hiyo—

Mara nyingi mambo yanayoandikwa katika wiki/wikipedia yanakuwa ni ya ukweli lakini hata baadhi ya muda yanakuwa yana chembe chembe za uwongo kwani kila mtu anaweza andika lolote katika ukurasa huo huo mmoja

Hivi ushawahi kujiuliza ni nani au ni kitu gani ambacho kinahaririwa sana katika mtandao wa wikipedia? Mtandao wa wikipedia mpaka sasa una makala zaidi ya 4,964,779 za kiingereza tuu na makala milioni 35 katika lugha 288 tofauti tofauti (ambazo sio katika lugha ya  kiingereza).

SOMA PIA  Facebook yapoteza wateja kutokana na GDPR

Kurasa mpaka ijichukulie umaarufu wa kuhaririwa sana ni lazima iwe na mambo mapya yanayojitokeza mara kwa mara sio? ndio! lakini unaweza shangaa hata kurasa ambazo hazina taarifa mpya (za kale) zinapata kuhaririwa sana.

Katika utafiti uliofanywa na Bw. Ramiro Gómez, ambae ni ‘developer’ wa ‘sofware’ anaekaa Berlin, umekuja na majibu ya swali letu juu ya kurasa zipi zinahaririwa sana katika wikipedia. Bw Ramiro Gómez alitumia mda wake katika kukusanya taarifa mbalimbali juu ya jambo hili

SOMA PIA  Vodacom Tanzania yazindua mfumo wa mawasiliano wenye kasi ya 5G nchini.

Mpaka sasa anaeongoza kuhaririwa sana ni raisi mstaafu wa marekani Bw. George W. Bush. Unaweza pia shangaa licha ya listi kuwa na Timu za michezo/wanamichezo kama vile Real madrid, Roger Federer na kuwa na Michezo ya Video kama vile PlayStation 3 na  RuneScape lakini mwanamke ni mmoja tuu Britney Spears, ambaye amejitokeza katika list hii ya watu/vitu 30 vinavyoongoza kuhaririwa katika mtandao wa wikipedia

SOMA PIA  Fairphone 2: Dondosha Simu Hii Kadri Unavyoweza! #Uchambuzi

Pata Habari Picha Juu Ya Kurasa Zinazoongoza Kuhaririwa Katika Wikipedia!

Kurasa Zinazoongoza Kuhaririwa Katika Wikipedia!

Kurasa Zinazoongoza Kuhaririwa Katika Wikipedia!

Listi haimaanishi kuwa itaendelea kubaki kuwa hivi hivi kumbuka watu bado wanaendelea kuhariri kurasa. Baada ya muda usishangae kuona kila kitu kimebadilika. Tuambie je ulikua unadhania namba moja atakuwa raisi wa zamani? Tuandikie sehemu ya comment. Ningependa kusikia kutoka kwako. Tembelea mtandao wako pendwa na namba moja kwa habari za teknolojia kila siku. TeknoKona Tupo Nawe!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania