Unaweza kuwa na akaunti yako ya Facebook lakini hukufahamu kuwa kuna ukomo/idadi ya mwisho kabisa kwa kila mwenye akaunti; ni marafiki tano elfu tu ndio akaunti moja inaweza kuwa nayo.
Unajua walimwengu walivyo kwenye kila kikwazo basi lazima atatafuta namna ya kutatua tatizo husika/kulitafutia ufumbuzi na kwa hali ya kawaida kama umeshafikisha idadi ya marafiki elfu tano basi haiwezekani tena kutuma maombi ya urafiki lakini ukweli ni kwamba njia ipo na inafanya kazi.

Ujanja wa kufanya kuomba urafiki hata kama akaunti yako imeshafikia kikomo.
Intaneti ndio msingi wa kila kitu wakati unaperuzi mtandaoni basi unachotakiwa kufanya ili uweze kutuma maombi ya urafiki kwa wewe ambae tayari una marafiki elfu tano fanya hivi:
Ingia kwenye akaunti yako ya Facebook, ukiwa kwenye ukurasa wa nyumbani/umeshamtafuta yule unayetaka kumuomba urafiki sasa zima kipengele cha kuruhusu intaneti halafu rudi kwenye akaunti yako kisha bofya Add Friend ili kutuma maombi ya urafiki kwa mhusika.