fbpx

Kamera, simu, Teknolojia

Simu ya mkononi ya kwanza kuwa na kamera

simu-ya-mkononi-ya-kwanza-kuwa-na-kamera

Sambaza

Watumiaji wengi wa simu rununu moja sifa za ni uwepo wa kamera nzuri ndani ya simu wanayotaka kununua halafu mengine ndio yaangaliwe.

Kuwepo kwa kamera kwenye simu za mkononi kumeongeza thamani sana na kuifanya kuwa moja ya kitu muhimu zaidi katika simu za mkononi. Aidha, uwepo wa kamera ndani ya simu kumepunguza kwa kiasi kikubwa biashara ya kamera, kujua zaidi>>BOFYA HAPA.

Umeshawahi kujiuliza ni simu gani ya mkononi ipo kwenye historia kwa kuwa simu ya kwanza kuwa na kamera? Sijui kama ulipata majibu lakini leo hapa teknokona tutakufahamisha kinagaubaga.

SOMA PIA  BRELA: Usajili wa Kampuni na Biashara sasa kwa Mtandao

Simu ya J-SH04 inatajwa kuwa ndio ya simu ya mkononi ya kwanza kuwa na kamera ndani yake. J-SH04 iliundwa na kampuni ya Japan ya Sharp Corparation.

Simu ya mkononi
Simu hii ilizinduliwamwezi Novemba mwaka 2000 na ilipatikana kwenye soko la Japan pekee. Kamera ya J-SH04 iliweza kuchukua picha za rangi za 0.11 Mega pixel.

Simu hiyo ya kisasa zaidi kwa wakati huo ilipata mafanikio makubwa sana kiasi kwamba mwezi mmoja baadae kulitolewa toleo lingine la J-SH05.

Simu ya mkononi
Sharp J-SH05; toleo la pili baada ya Sharp J-SH04.

Ujio wa simu hiyo ulifuatiwa na simu kutoka Samsung ya J-SH04 iliyokuwa na kamera ndani yake. Baada ya hapo ikafuatiwa na Sanyo SCP-5300 (2002), Audiovox PM8920 (2004) na Nokia N90 (2005).

Baada ya hapo maboresho ya ubora wa kamera ndani ya simu za mkononi yalianza kufanyiwa kazi mpaka kufikia sasa.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza
Tags: , ,

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.