Kwa mtu ambaye haoni ni ngumu kuelewa mengi juu ya mitandao hii ya kijamii, ni ngumu kwake kufurahia haya ambayo sisi tunafurahia, kwa kutambua haya Facebook wameamua kuleta huduma ambayo itawasaidia watu wasioona kuweza kuelewa picha zilizowekwa katika mtandao huu zinahusu nini.
Facebook wamekuja na programu ya artificial intelligence ambayo inazifanya server za mtandao huo ziweze kuelewa picha zinazopostiwa zinavitu gani na kuweza kuzisaidia programu zinazowasomea wasioona kuweza kusoma hata taarifa zilizo katika picha.
Kwa kawaida wasioona wanatumia programu ambayo inaweza kusoma maandishi yaliyo kaitika mtandao na kuyabadilisha kuwa katika mfumo wa maneno ya kusomwa hivyo kumuwezesah mtu asiyeoona kuelewa taarifa fulani, program hizi zilikuwa haziwezi kusoma taarifa ya picha hivyo kwa msaada huo wa picha katika mtandao wa facebook zitaweza kuwa gunduliwa na program maalumu na kisha taarifa yake kusomwa na program maalumu kwaajili ya wasioona.
Facebook inafanya hivi katika harakati za kuongeza watumiaji hai na hasa wakiwa wanalilenga kundi la watu wenye ulemavu wa kuona, picha ni moja kati ya vitu ambavyo vinatawala mitandao ya kijamii na inakadiriwa kwamba kila siku moja kuna walau picha bilioni moja na zaidi zinatumwa kila siku katika mitandao ya kijamii.
Program hii ya Facebook imefunzwa kutambua baadhi ya vitu mpaka sasa na siku zinavyoenda itazidi kufunzwa kutambua vitu vingi zaidi, vitu ambavyo programu hiyo inaweza kutambua mpaka sasa nipamoja na mazingira, vifaa vya usafiri, michezo chakula na muonekano wa watu.
Huduma hii inaanza katika vifaa ambavyo vinaendeshwa na iOS na pengine baadaye itakwenda katika Facebook ya kwenye Android, Muhandisi wa Facebook Matt King ambaye ni kiongozi katika ubunifu huu alipata upofu baada ya kupata ugonjwa wa macho na kwa uvumbuzi huu Matt atabadilisha namna mitandao ya kijamii itafanya kazi hasa kwa wasioona.
Huduma hii huenda ikasambaa katika mitandao mingine ya kijamii, maana mitandao kama Twitter wamekwishaanza kuonesha dalili za kuanza kuitumia teknolojia kama hiyo.
Makala hii imeandikwa kwa msaada wa mitandao ya BBC pamoja na The gurdian