Japokuwa waliiweka katika soko la Google Play siku wa wajinga duniani ( Aprili 1) bado App hiyo haikuwa na maisha marefu katika soko hili, kwani ilitolewa baada ya siku chache.
Google wamejitetea kwa kusema kuwa waliondoa App hiyo kutokana na kuwa ilikuwa ikikiuka sera zao za App. App hiyo ilikuwa inakwenda kwa jina la Alemarah
App hiyo ilikuwa ikihusisha vitu kama vile taarifa rasmi kutoka katika kundi hilo la kigaidi na hata baadhi ya video kutoka katika kundi hilo
Taarifa nyingi zilizokuwa zinatoka kupitia app hiyo zilikuwa zinatolewa kwa kutumia lugha ya Pashto na lengo kuu lilikuwa ni kushambaza taarifa kwa watu wengi haraka iwezekanavyo.
App hiyo ilitolewa katika soko hilo Aprili 2 huku wataliban wakiwa na uhakika kuwa ni tatizo la kiufundi kumbe mtandao wa Google ulikuwa ushafanya yao. Mbali na hapo Taliban walisema kuwa dhumuni kuu la kuwa na App hiyo ni moja kati ya mbinu za kuwa na wafuasi wengi kupitia Nyanja ya Teknolojia.
Bado Google hawajatoa taarifa rasmi juu ya kwa nini mtandao huu umeamua kuitoa app hiyo katika soko lake maarufu dhidi ya kujitetea kwa kusema App hiyo imekiuka sera zake ambazo zinaongoza Apps zote kwa ujumla. Watu na vyanzo vingi vya habari bado vinahisi kuna mambo zaidi nyuma ya pazia.
Sio Google tuu ambao wamejaribu kuzuia ushambazaji wa taarifa kutoka Taliban kwa njia ya Teknolojia. Taliban mwanzoni walikuwa wakitoa taarifa (Hata zile za vitisho) kwa kutumia mitandao ya kijamii kama vile Twitter na Facebook ambazo zilikua zikibainika zinazuiliwa mara moja. Tovuti ya mtandao huo wa Talban mpaka sasa una lugha zaidi ya 4 ambapo kiingereza ni moja kati ya lugha hizo.
Hii ni hatari sana kwa watu ambao wanaweza wakatekwa kirahisi na kuweza kujiunga katika michakato ya kundi hili ambalo ni tishio kubwa sana duniani. Kundi hili kwa kifupi lina serikali na misingi yake inayoliendesha kundi hili.