fbpx
apps, instagram, Snapchat, Teknolojia

Instagram Yaja Na ‘Sticker’ Kama Snapchat!

instagram-yaja-na-sticker-kama-snapchat
Sambaza

Licha ya kuwa watu wengi wanasema kuwa mtandao huo umekua ukiiba (ukinakili) vipengele mbalimbali kutoka snapchat bado hili halijawashusha kasi yao.


Mpaka sasa kampuni bado inafanya juu chini ili kuhakikisha kuwa watumiaji wa mtandao huo wanatumia kile kilicho bora zaidi.

Kampuni imekuja na sticker ambazo mtu unaweza ukaziweka juu ya picha au video yako. Sticker hizi zinatofautiana kwani zinakuja kwa aina tofauti tofauti.

INAYOHUSIANA  Tanzania Inaongoza kwa bei nafuu katika huduma ya intaneti Afrika- ‘Ripoti'

Kwa haraka haraka kuna zile sticker tulizozizoea zile za maeneo na zingine za Viemoji. Zote hizi katika mtandao wa Instagram.

Kingine cha kushangaza ni kwamba mtandao umetoa taarifa yake na kusema kuwa kwa siku watumiaji wa mtandao huo hutuma Story milioni 200 wakati mtandao wa Snapchat kwa siku ni story 160 tuu zinazotumwa.


Hapa ni wazi kuwa kampuni ya Instagram imeshaipiku Snapchat?

INAYOHUSIANA  Matunda ya Ubia wa Blackberry na Emtek: BBM kunufaika?

Aina ya sticker hizo ni Pinning And Selfie Sticker na Geosticker. Aina hizi mbili ya Sticker ndizo zitakazokuwa zinatumika katika mtandao wa Instagram.

Kama kwako bado hujaanza kupata huduma hii basi huna budi kusubiria sasisho jipya kabisa punde tuu pale linapotoka.

Tembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com