Inatokea mara nyingi kwa watu mbalimbali, unajishangaa unapitia katika mtandao wa TeknoKona huku unafanya mambo yako mengine kama vile kusikiliza muziki mara unashangaa kompyuta yako imeganda bila hata ya tahadhari yoyote
Unachezesha Mouse lakini wapi, kitu kimegoma! Saa nyingine hata unabofya vibonyezo mbalimbali katika keyboard lakini bado. Usitoe jasho, ngoja nikupe njia ya kushindana na jambo hili.
Restart
Sawa pengine hili linajulikana kwa kiasi kikubwa. Japokuwa wengine wanazani ni kuchomoa waya wa umeme kifaa kikizima wakiwashe tena. Usifanye hivyo jaribu kushikilia kitufe cha kuzima kwa sekunde 5 mpaka 10, bila shaka kifaa chako kitaji ‘Restart’
Kuna mambo mengi yanweza yakajitokeza wakati kompyuta yako inawaka. Kwa leo ngoja tuangalia yale ambayo yanatokeaga san asana.
– Kompyuta Inawaka Bila Tatizo Lolote
Hii inaweza ikawa siku yako, kama kompyuta yako ikiwaka salama kabisa kitu cha kwanza kufanya ni kuhifadhi taarifa zako za muhimu (Back Up). Hii itakuwa ni njia nzuri hasa kama kuna tatizo lingine ambalo lipo njiani, hii itakusaidia sana kuliko kuhangaika kupata taarifa zako katika kompyuta ambayo imekufa.
Baada ya hapo tumia kompyuta yako kama kawaida tuu pengine mpaka itakapo ‘freeze’ tena, japokuwa inaweza isifanye hivyo tena. Kama ikifanya hivyo endelea kusoma njia nyingine
– Kompyuta Inakuuliza Jinsi Ya Kuwaka
Unakuwa una ‘Restart’ kompyuta yako inaweza ikasema kulikuwa na tatizo katika Windows na inaweza ikakuuliza kama unataka kuiwasha katika hali ya kawaida au kwa kutumia njia ya tahadhari ( Normally Au Safe Mode). Kwa mara ya kwanza kabisa chagua Normally na kisha fanya hifadhi (Back Up) ya taarifa zako za muhimu. Kisha tumia kompyuta yako kama kawaida tuu na uangalia kama itaganda tena.
Kwa mara ya pili kama kompyuta yako imeganda chagua kuiwasha kwa njia ya usalama na tahadhari (Safe Mode). Kama ikiwaka basi kompyuta yako inaweza ikawa na tatizo la ‘Software’ au ‘Hardware’. Lakini usikate tama endelea kusoma unaweza ukapata ufumbuzi.
– Kompyuta Imeganda (Ghafla) Tena
Kama kompyuta ikiendela kuganda tena baada ya kutumia njia zote mbili za kuwasha yaani kuwasha kwa njia ya kawaida na kutumia ile njia ya kiusalama (Safe Mode). Bila shaka hapo kompyuta yako inaweza ikawa na tatizo katika ‘Hardware’ au ‘Software’ ingawa mara nyingi linakuaga ni lile tatizo la Hardware.
Njia Ya Kukabiliana Na Matatizo Ya Software
Mara nyingine kuganda kwa kompyuta kunaweza kukawa kumesababishwa na programu ambayo haifanyi kazi katika kiwango chake cha ufanisi. Fungua ‘Task Manager’ nia rahisi bofya CTRL + SHIFT + ESC ili kuifungua na kisha chagua sehemu ya ‘Performance’ kama unatumia Windows 8.1 au 10 itakubidi uki ‘click’ katika eneo la ‘More Details’ katika upande wa chini wa Task Manager.
Anza kutumia kompyuta yako kama kawaida tuu lakini macho yako yawe katika eneo la CPU, Memory au Disk (ndani ya Task Manager). Kama kompyuta yako itaganda tena na moja kati ya maeneo hayo yana namba kubwa ukilinganisha na mengine basi hilo linaweza likawa ndio jibu lako. Lijue eneo ambalo lina namba kubwa na kisha ‘restart’ kompyuta yako kama kawaida
Mara hii chagua ‘Process’ ndani ya Task Manager. Kwa mpangilio wa CPU, Memory au Disk, chochote ambacho kilikuwa na namba kubwa mwanzoni wakati kompyuta ilipoganda kisha angalia kipi kitakacho tokea juu kabisa wakati kompyuta inaganda. Hii itakuambia ni software ipi inaleta shida. Ukishapata jibu lako unaweza kuamua kuifuta kabisa katika kompyuta yako au ukasasisha (Update)
Njia Ya Kukabiliana Na Matatizo Ya Hardware
Kabla ya kuikimbiza kompyuta yako kwa fundi husika jua kwamba kompyuta ambayo iliganda baada ya kuwasha kwa kutumia njia zote mbili yaani ile ya kawaida na ile ya kiusalama zaidi na ukiwa ushajaribu njia ile ya kukabiliana na hili kwa kuangalia katika software. Kama haya yote yameshindikana, basi tatizo linaweza kuwa katika ‘hard drive’, CPU yako inachemka sana, tatizo kwenye Memory au njia za kusambaza umeme zina matatizo. Lakini pia inawezekana tatizo likawa ni motherboard japokuwa tatizo hili ni mara chache sana.
Mara kwa mara kwa matatizo ya Hardware, kuganda kutaanza kidogo kidogo lakini kutaongezeka kidogo kidogo. Saa nyingine kunajitokeza wakati kompyuta ikiwa inafanya kazi sana lakini sio wakati ukiwa unafanya mambo ya kawaida kawaida.
Kama ukihisi hili limekukuta basi huna budi kumtafuta fundi anaehusika vizuri na maswala ya kompyuta na ukifika kule muulizie Yule wa Hardware. Huyu atakupa ufafanuzi zaidi na kisha atakusaidia katika kuhakikisha kifaa chako kinarekebishwa.
Baada ya kusema hayo nahisi utakuwa umepata mwangaza juu ya kompyuta yako. Naomba nikushauri kuwa mdadisi, dadisi mapema kabla tatizo halijawa kubwa kwani tatizo kubwa inamaanisha gharama kubwa. Usije ukatajiwa bei mpaka kompyuta yako ukaisusa bureeeeeeeeee!