Kama wewe ni mtumiajia/ulishawahi tumia simu za blackberry utakua unafahamu fika kuwa kwenye huduma ya intaneti kwa hapa nchini kidogo kuna ugumu. Inakubidi ulipie huduma spesheli ambayo itakuwezesha kufaidi internet ya simu hiyo. Huduma Hii inajulikana kama Blackberry Internet Service (BIS).
Jambo hili kuna baadhi ya watu linawachukiza, hata mimi kipindi wakati natumia Blackberry nilikua nauzika, lakini mmoja kati ya marafiki zangu akanipa njia. Naomba na mimi nipitishie maujuzi kama ifuatavyo. Cha msingi ni kufuata taaratibu kama zinavyoelezwa
- Kwanza kabisa hakikisha simu yako ya blackberry haina bando spensheli (BIS). Unganisha bando la kawaida (lile ambalo kila mtu anaweza jiunga, lenye dakika, sms na MB/GB).
- Baada ya kuvuka steji hiyo, kisha nenda katika eneo la ‘Options‘ mara nyingine ‘Advanced Options‘ na tafuata TCP/IP (Transmission Control Protocol/Internet Protocol). Itatokea sehemu ya ‘APN settings’
- Anza kwa kuweka alama ya tiki katika neno ‘APN Setting Enabled‘ kisha mbele ya neno APN: andika internet, sehemu ya password na username paache bila kujaza kisha ‘save’ mabadiliko hayo.
- Baada ya hapo utakua tayari umeshaunganisha internet kwa mfumo wa kawaida katika simu yako ya blackberry lakini kuna jambo moja muhimu la kufanya.. Nalo ni kuziruhusu Apps mbalimbali kutumia intaneti hiyo
- Cha kufanya nenda eneo la ‘Options‘ kisha tafuta ‘Application Management‘ kisha chagua Apps unazotaka kuziruhusu kutumia intanenti hiyo
- Bofya App (kwa mfano WhatsApp) ukiwa ndani ya Application management kisha ‘View Permissions‘
- Bonyeza hilo neno ‘View Permissions‘ na kisha weka ‘Allow‘ katika vipengele vitatu vitakavyotokea
Baada ya kufanya yote hayo kwa mtiririko ‘save’ mabadiliko hayo kisha ‘resart’ simu yako. Kurestart simu yako kirahisi bofya ALT na SHIFT ya upande wa kulia pamoja na DEL kwa wakati mmoja bila kuachia mpaka simu yako itakapojizima. Baada ya sejunde kadhaa itawaka na utaweza kutumia App zako kama kawaida kwa kutumia intaneti ya kawaida.
MUHIMU: Baada ya kutumia njia hizi na kupata intaneti hii, hautakuwa na uwezo wa kutumia App ya BBM kwani hiyo inatumika pale unapokuwa na BIS tuu
Mara nyingi hata baada ya kutumia njia hii bado ‘internet browser‘ (Kivinjari cha blackberry) huwa kinagoma /kinasumbua kufanya kazi. Cha msingi kabla ya kuanza kutumia njia hizi hakikisha kwanza umeshusha kivinjari cha opera mini katika simu yako maana utakifanyia maboresho kama App zingine baada ya kufuata njia hizo.
No Comment! Be the first one.