Ni majanga kumdanganya mwenzi wako…ila ni majanga zaidi pale ambapo mtandao unaoutegemea katika kukusaidia kuchepuka kisiri kuibiwa data kuhusu wewe na walio na taarfa/data hizo kusema wataziweka wazi mtandaoni. MAJANGA!
Teknolojia imerahisisha mambo mengi sana na uwezi amini ila ndio ukweli teknolojia sasa inatumika kuwezesha yote mazuri na mabaya kulingana na mtazamo wako binafsi.
Mtandao maarufu unaowawezesha watu walio kwenye ndoa au mahusiano kuwa na michepuko umeibiwa data muhimu kuhusu watumiaji wake – (www.AshleyMadison.com). Sifa kubwa katika mtandao huo wa Ashley Madison umekuwa ni usiri kwa watumiaji wake duniani kote, na jambo hili lipo katika wasiwasi wa kupotea kwa sasa kwani wakati wowote kuanzia sasa watu waliofanikiwa kuiba data wanaweza wakaweka wazi kuhusu watumiaji wa mtandao huo.
Data za watumiaji zitakuwa na taarifa muhimu kuhusu mtu, kwa mfano majina, mahali anapoishi na pia picha mbalimbali za faragha.
Kundi lilijitambulisha kama wao ndio wanye data hizo wamesema wanachotaka ni huduma hiyo kuondelewa kabisa. Yaani kama mtandao huo utakubali kujiondoa kibiashara na kufuta huduma yao basi data zinazohusu watumiaji wake hazitavujishwa mitandaoni, ila kama mtandao huo utaendelea kufanya kazi basi wao watavujisha data hizo.
Mtandao huo una watumiaji zaidi ya milioni 37. Je una maoni gani na tukio hili, tuambie.
No Comment! Be the first one.