Kampuni ya Vodacom masaa machache yaliyopita kupitia ukurasa wake wa Facebook wametangaza ofa kabambe kwa kipindi hichi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Kuanzia saa tano usiku hadi saa moja wateja wa Vodacom wataweza kupiga simu bure(Vodacom kwenda Vodacom) na kutuma ujumbe mfupi wa maneno(sms) bila kikomo baada ya kujiunga kwa gharama ndogo ya Tsh 250/= kwa siku. Na zaidi ya yote ni kuhusu utumiaji wa intaneti/mtandao, huduma ya intaneti katika masaa hayo itakuwa bure pia, bila kikomo (unlimited).
Wale vijana wa ‘mfumo wa torrents’ kama Vodacom wanavyosema siku zote ‘kazi ni kwenu’!
Kujiunga piga *102*250#
Kutoka Teknokona, nawatakia Ramadhan njema!
No Comment! Be the first one.