Apple na Samsung ni makampuni makubwa sana katika nyanya ya kiteknolojia, ukiachana na ufanyaji kazi wao pamoja katika maeneo mbalimbali bado wanabaki kuwa washindani.
Kwa miaka kadha wa kadha Samsung wao waliokua wanaongoza katika orodha ya mauzo ya simu janja nyingi huku Apple wakifuatia katika orodha.
Mchuano ni mkali sana kwa sababu kwa mwaka makampuni yote mawili hutoa simu janja ambazo zina sifa za aina yake na hakika huwa zinawavutia wengi.
Hii inakua ni mara ya kwanza kabisa tokea mwaka 2010 jambo hili kutokea –samsung kutolewa katika reli—na mtengenezaji mwingine wa simu janja.
Kwa taarifa hali zilizopo ni kwamba Apple imeweza kuuza vifaa 234.6 duniani kote huku mpinzani wake, Samsung yeye aliweza kuuza vifaa 226.6
Taarifa zingine ni kwamba zinaonyesha kwa Apple wao wana ukuaji mzuri sana kwa mwaka ambao unaonyesha mambo yao sio mabaya katika biashara yao.
Kumbuka kwa Apple wao bidhaa yao ambayo huwa inafanya vizuri sana katika soko kuliko nyingine ni iPhone.
Ripoti hizi zote ni kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa kwa mwaka 2023 tuu, huku taarifa hizo zikiwa zinaonyesha kuwa thamani ya Apple katika soko imefikia mpaka 20.1% huku ikiwa inaongoza orodha hiyo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je undhani kampuni hii wao wataweza kukaa katika nafasi hiyo kwa muda mrefu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.