Rekodi hii ilikua inashikiliwa na Apple kwa miaka kadhaa huku makampuni mengine yakiwa yanafutia, Microsoft wao walikua wanafuatia katika namba hiyo.
Sio Apple na Microsoft tuu, makampuni mengi ya kiteknolojia huwa yanafanya vizuri sana katika orodha za makampuni yanayofanya vizuri duniani katika orodha ya thamani.
Microsoft yenyewe kwa sasa imefikia thamani ya dola za kimarekani trilioni 2.89 huku Apple wao wakiwa na thamani ya dola za kimarekani trilioni 2.78.
Kingine kikubwa katika makampuni haya ni kwamba mara kwa mara huwa wanapokonyana hii nafasi ya kwanza katika orodha hizi.
Hii inaonyesha kwamba makampuni haya yana ushindani mkubwa sana na ndio maana hata hawapishani kwa kiwango kikubwa sana cha kutisha – japokuwa bado ni hela nyingi sana sio?
Ukuaji wa kampuni ya Microsoft vile vile inawezekani wazi wazi umetokea kwa haraka haraka baada ya kampuni hiyo kufanya uwekezaji mkubwa kama vile kununua makampuni mengine n.k
Kwa Apple wao wamekua wakipata shida katika kuhakikisha simu zao zinaendana na uhitaji wa wateja wao, nadhani umeona hata mauzo ya iPhone 15 yalivyokua tofauti kabisa na matoleo mengine.
Wataalam mbali bali wanadai kwamba kwa asilimia kubwa sana Microsoft imeweza kupata nafasi hiyo baada ya uwekezaji mkubwa katika teknolojia ya AI kama vile Copilot.
Kwa haraka haraka Apple na wenyewe wana vifaa vyao ambao wamejiandaa kuviachia mwaka huu kama vile Vision Pro ambapo pengine vinaweza kuirudisha kampuni kuwa namba moja
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je unadhani kampuni itashika nambo moja hivi karibuni au bado sana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.