Kwa wale ambao wanatumia iPhone/bidhaa za Apple watakuwa wanafahamu app ya Siri iliyo mahususi kwa kutoa msaada fulani. Kuiamuru programu tumishi ya Siri kupiga namba 108 si kitu cha mzaha! Fahamu sababu za undani wa namba 108 kwenye Siri.
Watu wenye kufanyia wengine mzaha wamekuwa wakiwahadaa wanaotumia simu za iPhone kutamka ‘108’ kwenye huduma ya kutambua sauti ya Siri.
Namba ‘108’ ina maana gani kwenye app ya Siri?
‘108’ ni sawa na ‘112’ nchini Tanzania, hivyo Siri inatafsiri hatua hiyo kama jaribio la anayetumia simu kupiga simu ya dharura na hivyo, hilo linaifanya kupiga mara moja simu ya dharura hadi kwa polisi au maafisa wa huduma za dharura.
Kwa wengine walio na utani uliovuka mipaka huwashauri wenye simu (iPhone) “kufunga macho sekunde tano” wanaposoma 108 😀 😛 . App ya Siri kawaida humpa mtu sekunde tano kubadilisha mawazo kabla ya kutekeleza agizo ulilolitoa.
Mzaha huu hufanya maafisa wa usalama kupoteza muda katika jambo ambalo si la dharula. Nchini Uingereza na Wales, unaweza ukatozwa faini ya hadi £80 (takribani Tsh 217,800) ilihali hakuna dharula yoyote.
App ya Siri ni app iliundwa kwa ajili ya kutoa msaada wa aina fulani hivyo si vizuri kuitumia app hiyo kimasihara na unaweza ukaangukia pabaya ila kama kweli unahitaji msaada wa dharula huna budi kusema ‘108’ wakti app ya Siri ikiwa inafanya kazi.
Vyanzo: The sun, Mirror, BBC
One Comment
Comments are closed.