fbpx
Kompyuta, Microsoft, Teknolojia, Windows 10

Microsoft yatoa vitu viwili kwa mpigo; Laptop na Windows 10 S

microsoft-yatoa-vitu-viwili-kwa-mpigo-laptop-na-windows-10s
Sambaza

Katika ile hali ya kuzidi kuleta ushindani katika biashara Microsoft imeamua kutoa vitu viwili kwa wakati mmoja ambapo kwa sababu iliyowazi kabisa ni kushindana na kompyuta za Chrome OS na Apple MacBook.

Windows 10 ambayo inaonekana kufanya vizuri na kuzidi kupata watumiaji wengi Microsoft wameamua kuleta toleo jingine la programu endeshaji kutoka familia ya Windows 10 na toleo hilo likiitwa Windows 10 S. Hata hivyo Microsoft haikuishia hapo kwani wametanganza kompyuta mpakato inayoenda kwa jina la Surface Laptop.

Nini kipya kwenye Surface Laptop?

WINDOWS 10 S
Pia Microsoft wanakuja na laptop ndogo zenye lengo za kutumika mashuleni kwa kutumia programu endeshaji ya Windows 10 S hizi zitalenga mashule na pia kushindana na laptop za Chromebook ambazo tayari zimeshikilia masoko ya mashule katika mataifa kama Marekani na ata Ulaya

Surface Laptop imewalenga zaidi wanafunzi wa vyuoni huku ikiwa ni nyepesi kuzidi kompyuta zote zilizowahi kutolewa na Apple. Lakini ikifanana baadhi ya vitu katika kompyta zilizotangulia (Surface Pro naSurface Book) kabla ya hii mpya. Surface laptop ina features kama:- kioo cha mguso na cha rangi chenye ukubwa wa ichi 13.5 na malighafi yake ya juu ikiwa ni ya fabric ambapo vitu hivyo vipo pia kwenye Surface Pro na Surface Book.

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kutumia Microsoft Office Bure! #Online

Mengineyo yaliyopo kwenye Suraface laptop.

Laptop hii mpya inakuja na wembaba wa mm 14.5, uzito wa kilo 1.25, sehemu ya kuchomekea headphones, waya wa chaji kitachokuwezesha kuunganishwa na mengineyo (accessories) yanayopatikana kwenye Microfoft. Surface laptop inatumia teknolojia ya USB Type A badala ya USB Type C ambayo imezoeleka katika simu na kompyuta zilizotoka miaka ya karibuni.

Surace Laptop ni nyembamba zaidi ya kompyuta za Google (Chromebook) au hata zile MacBook na huku ikiwa inatunza chaji muda mrefu zaidi ya kompyuta ya Google/Apple.

Soma pia: Microsoft na kompyuta za Surface

Surface laptop itakuwa inatumia programu endeshaji ya Windows 10 S (ila utaweza kuupgrade kwenda Windows 10 Pro ukitaka kwa dola 50 tuu) huku ikija na Intel Core i5 au i7 na uhifadhi wa mpaka TB 1, RAM ikiwa ni kuanzia GB 4 na ikiuzwa kuanzia dola za Kimarekani 999 (takribani 2,297,700 kwa shilingi za Kitanzania) kwa kompyuta yenye RAM ya GB 4, Core i5, diski uJazo wa GB128 SSD na zitaanza kupatikana Juni 15.

Kuhusu Windows 10 S

Kubwa kuliko ambalo limejumuishwa kwenye toleo jipya la Windows 10 S ni kutoruhusu programu tumishi ambazo hazikupakuliwa kutoka wenye Windows Store kufanya kazi. Microfoft wameamua kufanya hivyo ili kuongeza usalama, uimara na kasi ya kompyuta.

INAYOHUSIANA  Wanyama kuweza kubashiri tetemeko la ardhi. #Sayansi

Lakini pia hii inaonekana kutaka kushindana moja kwa moja na programu endeshaji ya Chrome OS inayotengenezwa na Google.

Je, una mtazamo gani juu ya vitu hivi viwili kutoka Microsoft? Kwetu tunadhani bado itakuwa vigumu kushindana na laptop za Chrome OS kwani laptop hizo huwa zinakuwa za bei nafuu sana, kwenye Tsh 300,000 – 500,000, unaweza pata laptop mpya kabisa ya Chrome OS.

Surface Laptop ingawa inavutia kwa sifa na ubora bado ni laptop ghali kwa watu wengi sana hasa katika nchi zinazoendelea.

Vyanzo: theGuardian, pamoja na mitandao kadha wa kadha.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|