Toleo la simu lijalo kutoka kampuni ya Apple, litakaloitwa iPhone 5 pamoja na tableti ya iPad Mini inayotegemewa kuleta ushindani zaidi dhidi ya tableti za Android, zinategemewa kuingizwa sokoni mwezi Septemba mwaka huu.
Mtafiti kutoka kampuni ya KGI Securities, Bwana Ming-Chi Kuo inasemekana simu na tableti hizo zipo katika hatua za mwisho kimatengenezo. Wakati huo huo kampuni ya Apple bado imekaa kimya kuhusu habari zilizoenea kuhusu kuja kwa iPad Mini.
iPad mini ndiyo itakuwa tableti ndogo kwa ukubwa kutoka Apple, na hii ni tofauti sana na msimamo wao wa muda mrefu tokea enzi za Marehemu Steve Jobs. Steve Jobs alishatamkaga kuwa kampuni hiyo haitatengeneza tableti ndogo za ukubwa wa nchi 7, maarufu kama ‘mini’, hii ni ikilinganishwa na tableti yake inayouza zaidi duniani, iPad 1,2 na 3 zote zikiwa na ukubwa wa nchi 10.
Picha ya Mfano Ikionesha iPad Mini (ya chini) |
Tableti zinazotumia Android kama Samsung, Acer, Huawei na zingenezo zimeweza kupanda sana kimauzo kutokana na kutoa matoleo ya ukubwa mdogo wa nchi 7, kwa bei rahisi, na inasemekana kampuni ya Apple imeona ni bora nao watoe toleo hilo kukidhi soko kubwa linalokua la kompyuta ndogo za tableti.
No Comment! Be the first one.