Tunaposema teknolojia inavuka mipaka na kurahisisha mambo hatukosei kabisa,
nafurahi kusema TeknoKona imepata logo mpya ya kuvutia kutoka kwa mbunifu kutoka nchini Italy anayeishi Ufaransa kwa sasa.
Ni rafiki yangu wa muda mrefu na mpenzi wa kazi za TeknoKona 😉
Bado anajifunza kiswahili bila hivyo anasema angependa kuchangia makala Teknokona…. nami nasema Hakuna Matata kabisa.
Huu ndo muonekano wetu kwa sasa,
mambo yanaelekea pazuri…
Hakika zinavutia, au mnasemaje?
Fabrizio Furchi ni mbunifu(Designer) na mtangazaji wa Radio anayetokea nchini Italia na sasa anafanya kazi nchini Ufaransa. Ashawahi kufanya kazi ya kujitolea Tanzania miaka ya nyuma, na bado ana mapenzi sana na nchi yetu. Anaweza patikana kupitia twitter @SpaceChili na Google Plus kwa kubofya hapa!
No Comment! Be the first one.