fbpx
Kompyuta, Maujanja, Teknolojia

Namna ya kufunga nyaraka kwa nenosiri

namna-ya-kufunga-nyaraka-kwa-nenosiri
Sambaza

Usalama kwenye maisha yaliyotawaliwa na teknolojia ni kitu muhimu sana hasa pale unapopenda kuwa mtu wa kutopenda kuweka mambo yako wazi na katika zama hizi za kidijitali matumizi ya nenosiri si jambo la ajabu.

Katika maisha ya kwenda na teknolojia siku hizi ni mara chache mtu kutumia kalamu na karatasi kuandika nyaraka na badala yake kompyuta kupitia programu wezeshi imekuwa ikifanya kazi hiyo. Sawa, umeandika barua yako lakini suala linakuja pale ambapo unataka kuweka ulinzi ili kwa mtu yeyote atakayetaka kuifungua basi akutane na kizingiti. Je, utafanyaje?

INAYOHUSIANA  BitCoin yazidi kung'ara; thamani yake yazidi kuongezeka

Jinsi ya kufunga nyaraka kwenye Ms. Word 2010/2013

Kwanza kabisa ni kufungua programu husika (Microsoft Word 2010) kisha unaanza kuandika unayoyataka kuyaweka kimaandishi na baada ya hapo inafuata hatua ya kutunza nyaraka kwa lengo la kuweza kuipata kiurahisi pale utakapoihitaji kwa mara nyingine tena. Sasa mara bada ya hilo kukamilika tutazame ukurasa wa pili: Namna ya kuifunga nyaraka kwa nywila.

 • Ndani ya Ms. Word nenda kwenye File > Info > Protect Document > Encrypt with Password,
 • Weka nenosiri (nywila) unalotaka kisha bofya OK,
 • Rudia nywila uliyoweka kwenye hatua ilyopita halafu bonyeza OK kwa mara nyingine tena na hapo utakuwa umeiwekea ulinzi nyaraka husika kwa kutumia nywila.
  kufunga nyaraka
  Habari kwa picha: Nmna ya kuweka nenosiri kwenye nyaraka.
  kufunga nyaraka
  Hatua namba 2 ya namna ya kufunga nyaraka kwa nywila.

   

Kama unatumia Ms. Word 2007 kwenye kompyuta basi hatua za kufuata ni kwenda kwenye File > Prepare > Protect Document > Encrypt with Password. Maelezo yanayofuata baada ya hapo yanafanana na hayo niliyoyaeleza awali.

kufunga nyaraka
Namna gani unaweza kufunga barua kwenye Microsoft Word 2007.

ANGALIZO! Kila kitu kina faida na hasasra zake sasa unaweza ukafurahi kuwa umeweza kuweka nenosiri kwenye nyaraka lakini kumbuka UKISAHAU NYWILA haitawezekana tena wewe kuweza kuiona bila ya kuifungua kwa aina hiyo ya ulinzi.

Chanzo: Microsoft

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

 1. Kulinda faili ndani ya Windows 7, 8 au 10 - TeknoKona Teknolojia Tanzania
  May 19, 2020 at 7:30 pm

  […] baada ya kuweka hewani makala inayohusu jinsi ya kuweka nenosiri kwenye nyaraka mmoja wa wasomaji wetu akauliza swali lililosababisha kufikiria kuandaa somo hili kwa faida ya […]