Google imetoa onyo kwa watengeneza programu kwamba wanahitaji kuwa wazi na watumiaji kuhusu maelezo wanayoshiriki na Huq, kampuni ya Uingereza inayouza taarifa. Google imesema programu ambazo hazifuati sera zao za data zitapigwa marufuku kwenye Play Store.
Hali hii imetokea baada ya Huq kukiri kwa BBC kwamba angalau washirika wawili wa programu hawakutafuta ruhusa sahihi za watumiaji. Huq alisema kampuni hiyo ilichukua swala la ulinzi wa data “kwa uzito sana” na inaamini kuwa washirika wote sasa wanafuata sheria.
Ushirikiano wa programu za kushiriki data na wahusika wengine unachunguzwa zaidi na wadhibiti na watunga sera duniani kote. Huq inashirikiana na programu nyingine nyingi, ikijumuisha programu ya maombi ya Waislamu, programu ya kufuatilia safari za ndege na programu ya hali ya hewa.
Watengenezaji na wamiliki wa programu hupachika baadhi ya mistari ya maneno yaliyotolewa na Huq ambayo hutoa data ya eneo – ambayo Huq hukusanya. Taarifa hizi kisha huuzwa kwa wateja, ikijumuisha mabaraza mbalimbali ya Uingereza. Makala iliyoandikwa Oktoba na Vice iliibua shaka iwapo watu walijua kuwa taarifa ilikuwa ikishirikiwa walipotumia programu hizi.
Huq ilikiri kwa BBC kwamba angalau programu mbili ziligawana taarifa na kampuni hiyo, bila kutafuta kibali sahihi kutoka kwa watumiaji. Oktoba, Google ilianzisha sera mpya ya data ya mtumiaji ikifahamisha programu kwamba lazima ziwe wazi kuhusu jinsi data yoyote wanayokusanya inatumiwa.
Google ilisema: “Kama sehemu ya uchunguzi wetu, tumetuma onyo kwa watengeneza programu wote ambao tulibaini kuwa wanakiuka sera za Google Play.” Lakini ilikataa kusema ni watengeneza programu wangapi walipokea onyo hilo.
Mtendaji mkuu wa Huq Conrad Poulson alisema: “Tunaendelea kuchukua suala la ulinzi wa data na idhini kwa umakini sana na kuunga mkono kikamilifu mpango wowote ulioundwa kufanya maboresho katika suala hili.
“Ni muhimu sana kwetu kwamba tuendelee kufanya kazi pamoja na washirika wetu ili kusaidia kuhakikisha mbinu bora za faragha zinatekelezwa na kudumishwa.”
Chanzo: BBC na vyanzo vingine.
No Comment! Be the first one.