Facebook imesema kwamba inafanya kazi uwezo wa kuwatag marafiki zako walio katika video zako moja kwa moja yaani automatically (ku-auto tag), hii itawaondolea watumiaji uhitaji wa kuanza kutafuta marafiki na kuwatag baada ya kusambaza video.
Facebook inaamini zaidi katika picha na video kuwa ndiyo njia kuu ya kufanikiwa katika mtandao wa kijamii, hii inawafanya wajitahidi kwa kila uchao kuhakikisha kwamba wanatengeneza mazingira ya watu kufurahia huduma za picha na video.
Katika mkutano wake wa ma-developer Facebook wamesema wanafanyia kazi auto-tag feature ambayo itawasaidia watumiaji wa video kuweza kusambaza video kwa marafiki zao kirahisi zaidi.
Joaquin Quiñonero Candela ambaye ni bosi katika kitengo cha machine learning anasema kwamba wazo ni kwamba mtumiaji aweze kutafuta watu katika video ambazo marafiki walizisambaza.
Tuseme nimesambaza video ambayo mimi na rafiki yangu tukiongea katikati ya mazungumzo anakuja rafiki yetu mwingine naye anajiunga, hii video ikisambazwa na kisha mtu aka- search jina la rafiki yetu basi video itakuja na itaanzia katikati pale ambapo rafiki yetu watatu anaingia katika mazungumzo.
Facebook wako katika ushindani mkubwa na mitandao mingine hasa Snapchat ambao nao kila kukicha wanakuja na huduma mpya za kuwavutia wateja.
Vyanzo: Makala hii imeandikwa kwa msaada wa mtandao wa TECHCRUNCH na mitandao mingine