Profesa Stephen Hawking mwanakosmolojia (Watu ambao wanasomea juu ya uundwaji wa ulimwengu) anayeheshimika duniani kwa mchango wake mkubwa leo amejiunga na mtandao wa Weibo ambao pia unachukuliwa kuwa ndio Twitter ya china, na ndani ya sikumoja tayari amekwisha jipatia zaidi ya wafuasi milioni moja.
Hawking ni profesa ambaye hakuwahi kukubali ulemavu wake uwe kikwazo cha yeye kufanya mambo makubwa katika ulimwengu wa fizikia, Matatizo yake ya kiafya yalimsababishia apoteze uwezo wake wakuongea lakini hili pia halikumsimamisha kuongea kwani kwa sasa anatumia kompyuta kuongea.
Hawking amepata washabiki wengi katika mtandao huo maarufu wa china na hata kumshinda bosi wa Apple ambaye pia yupo katika mtandao huo kwa mwaka mmoja sasa. Inasemekana kwamba profesa huyu anapata mashabiki wengi China kutokana na tabia ya wachina wengi kuheshimu watu wenye mafanikio ya kitaluuma kitu ambacho Mwingereza huyo anaheshimika nacho.
Hawking alipokewa kwa furaha nawatumiaji wa mtandao huo ambao walitumia #HawkingOpensaWeibo ambayo ilikuwa ni moja ya hashtags ambazo zilitajwa zaidi katika mtandao huo siku ya jana.