fbpx
apps, Mtandao wa Kijamii

TikTok: App iliyokuwa kwa kasi mwaka 2019, tishio kwa Facebook

tiktok-app-iliyokuwa-kwa-kasi-mwaka-2019-tishio-kwa-facebook
Sambaza

TikTok ni app inayowezesha watumiaji wake kutengeneza video fupi na kuweza kutazama za wengine na kushiriki kwenye mashindano ya video yanayohusisha sauti au jambo flani.

Data zinaonesha nje ya apps zinazomilikiwa na Facebook, app ya TikTok ndio app iliyofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2019.

app ya tiktok
App ya TikTok inamilikiwa na kampuni ya ByteDance ya nchini China

Tovuti ya data na utafiti ya Sensor Tower imesema hadi sasa app ya TikTok imeshafikisha zaidi ya downloads bilioni 1.5 kwenye masoko ya app ya App Store (iOS) na Google Play. Kwa ujumla, TikTok ilishika nafasi ya 3 nyuma ya WhatsApp na Messenger kwa jumla ya downloads. Kwa mwaka 2019 app hiyo ilipata downloads nyingi kuzidi app za Facebook na Instagram ambazo zilishika nafasi ya nne na tano.

Kwa mwaka 2019 app hiyo iliifunika app ya Instagram kwa tofauti ya zaidi ya downloads milioni 238.

Instagram walifikisha wastani wa watumiaji bilioni 1 kila mwezi mwaka 2018, TikTok walifikisha idadi hiyo mwezi Juni 2019. Inasemakana kwa sasa tofauti yao inaweza ikawa ni ndogo sana, na kwa mwaka 2020 inawezekana kabisa TikTok kuwapiku Instagram.

INAYOHUSIANA  Twitter yaongeza idadi ya herufi za majina za watumiaji wa Twitter #Masasisho

Kizazi kipya – Facebook vs TikTok

Ukuaji wake wa haraka unaleta wasiwasi kwa mtandao wa Facebook. Kwa muda sasa Facebook wamekuwa na wakati mgumu kuweza kuhakikisha mtandao wao wa kijamii unaendelea kuvutia watumiaji wenye umri mdogo, kizazi kipya. TikTok kwao hali imekuwa tofauti, kizazi kipya ndicho kinachoendesha ukuaji wake wa kasi duniani kote.

Machache kuhusu TikTok:

  • App hii inatumia mfumo wa ‘Follow’, ambao upo pia Instagram na Twitter
  • Sio lazima wewe uweke vitu vyako, unaweza kujiunga kwa ajili ya kufuatilia akaunti utakazozipenda.
  • Baadhi ya video maarufu kwenye TikTok ni video za uchekeshaji, zinazoweza tengenezwa na mtu yeyote
  • App inakuja na uwezo mkubwa katika eneo la kufanya mabadiliko (edit) ya video, utaweza kuongeza na kubadilisha mambo mengi

Soma habari za apps mbalimbali -> Teknokona/Apps

Je upo TikTok tayari? Una mtazamo gani kuhusu app hii kwa sasa?

Vyanzo: Business Insider na tovuti mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |