Mambo mengi hivi sasa ni kama hayapo vile lakini kumbe athari zake bado zipo palepale na hii inatokana na dunia kuweka nguvu zaidi kwenye mapambano dhidi ya Virusi vya Corona ambapo nchi nyingi tuu ulimwenguni suala zima la kupunguza maambukizi ni kitendawili ambacho bado hakijateguliwa.
Katika ulimwengu wa kidjiti tuna uwezo wa kupata taarifa kwa njia mbalimbali mojawapo ikiwa ni kwa tovuti ambapo ziamua kutoa elimu ya kujikinga na virusi hivyo ambavyo mpaka sasa vimeshagharimu maisha ya mamilioni ya watu duniani.
Facebook ni moja ya mtandao wa kijamii wenye watumiaji wengi zaidi ulimwenguni imewezesha watumiaji wake kuweza kuchapisha taarifa mbalimbali zinazohusu virusi vya Corona lakini sasa wameweka klitu ambacho binafsi nakiita “Jicho la pili“. Iko hivi:
- unapotaka kuchapisha habari kuhusu virusi vya Corona Facebook wameweka mfumo ambao utakwambia kuwa taarifa hiyo chanzo chake ni tovuti fulani hivyo unaweza kwenda kujiridhisha kwanza kabla ya kuamuru iende hewani (watu/marafiki zako waweze kuiona). Hii inajumisha kufahamu zaidi chanzo chake, taarifa hivyo ilichapishwa lini kwa mara ya kwanza pamoja na mambo mengine,
- taarifa ambazo chanzo chake ni mamlaka zinazofahamika duniani mfano Shirika la Afya Duniani au mamlaka mbalimbali kutoka nchi husika (serikali, Wizara ya Afya, n.k) mhusika hatakuwa akipewa maelezo ya kwenda kuhakiki kwanza kabla ya kuirusha mtandaoni kwa sababu machapisho hayo yamewekwa kwenye kundi ambalo kuaminika zinapotoka.
Si jambo mbaya kuweka taarifa zinazohusu virusi vya Corona kwenye mitandao ya kijamii lakini tujiridhishe kwanza tulipozitoa kabla ya kuzipeleka kwa wengine ili kuepuka upotoshaji na pengine kuwa salama na mkono wa sheria.
Vyanzo: Gadgets 360, Media Post