fbpx

Apple yapunguza bei ya betri ya simu zake

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Betri za simu za Apple daima zimekuwa si bei rahisi lakini mwaka unaisha huku wakilazimika kupunguza bei ya betri za simu janja kutokana na makosa yao wenyewe kwenda kwa wateja wake.

Siku kadhaa zilizopita Apple iliachia sasisho fulani kwenda kwenye simu zake (iPhone) jambo lilipelekea utendaji wa kazi kwa iPhone 6, 6S, 7 na SE kwa betri ambazo ni za muda mrefu kufanya simu hizo kuwa nzito na kutumia kiwango kikubwa cha chaji kutokana na sasisho hilo.

Apple imepunguza bei ya betri za simu zake kwa $50 kutoka $79 (Tsh. 177,750) mpaka $29 (Tsh. 65,250) kutokana na kuruhusu sasisho ambalo limesababisha karaha bila kujali madhara/faida ya maboresho waliyoyatoa.

Betri ya iPhone 7: Prosesa ya kwenye simu inapohitaji umeme zaidi kuliko kile kiwango ambacho betri ina uwezo wa kutoa simu huzima bila kutarajia.

Baada ya sasisho hilo kuruhusiwa lilipelekea simu za iPhone ambzo betri zake ni za muda mrefu kupelekea simu kuzima bila kutarajia kutokana na betri hizo za Lithium kutopokea uwiano mzuri wa kiwango cha nguvu kwa betri husika.

Apple imekiri na kuomba msamaha kutokana na kusababbisha baadhi ya simu za wateja wake kutofanya kazi vizuri mpaka pale walipobadilisha betri kwenye simu zao. Kwa mujibu wa tamko walitoa wanasema hawakuwa na nia mbaya kwa wateja wa simu zilizoathiriwa kutokana na sasisho hilo.

INAYOHUSIANA  Samsung J7 Inaweza Kuwa Ya 1 Kuja Na Kamera Mbili Za Nyuma Kutoka Samsung!

Wapo baadhi ya wateja waliamua kuwafungulia Apple mashtaka na kama mojawapo ya kurekebisha kosa lao wamepunguza betri ya simu hizo lakini wapo wanaohoji kama isingebainika kuwa sasisho hilo ndio tatizo si wangeendelea kutoa vitu bila taarifa?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.