Apple ni moja kati ya kampuni ambayo imekua ikisemwa sana kuhusina na chaja ya vifaa vyake vya iPhone na iPad kutofautiana na vifaa vingine.
Licha ya kuwa kwa sasa vifaa vingi sana vinatumia teknolojia ya kuchajia ya USB tena ile ya Type-C lakini bado si kwao Apple na hili wamelithibitisha wao kwamba linakwenda kubadilika.
Kwa taarifa iliyo rasmi kabisa Apple imekiri kuwa itaanza kutumia chaja zenye tundu hilo –jipya kwao – japokuwa timu nzima haina furaha kutokana na uamuzi huo.
Unaweza ukawa unajiuliza ni kwanini kampuni hii inalazimika kufanya maamuzi ambayo hata wao wenyewe hawayapendi (hawafurahishwi nayo) lakini utagundua ni kwamba kinachofanya hivyo ni sharia/maamuzi ambayo yamewekwa na nchi za ulaya.
Kwa nchi za ulaya imepitishwa kwamba wawe wanatumia USB Type-C katika simu zote, tabiti zote na kamera zote na hii ni mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2024.
Na hili kuna hati hati kubwa likawezeshwa mpaka katika kompyuta mpakato (laptop) zote mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2026.
Kwa haraka haraka jambo hili linasaidia hata katika swala zima la kupunguza uchafu wa kielektroniki katika mazingira na vile vile inasaidia watu kuwa na machaguo ya muda mrefu.
Licha ya Apple kuwa mbishi kwa kipindi cha muda mrefu sana katika kuhakikisha kuwa anajitegemea kwa kila kitu safari hii hana ujanja tena, inabidi tuu aendane na hali halisi
Ningependa kusikia kutoka kwako, wewe unadhani ni sawa kwa kampuni ya Apple kuingia na kuanza kutumia chaja zile za USB Type-C?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.