fbpx
Uchambuzi

FAHAMU: Aina Za USB Na Matumizi Yake!

aina-za-usb
Sambaza

Kama umeshawahi kuhamisha taarifa kutoka kifaa kimoja cha kieletroniki kwenda kingine basi kwa namna moja au nyingine umekwishatumia teknolojia ya USB kukamilisho kitendo hicho.

Universal Serial Bus (USB) za kwanza kwanza kabisa zilianza katika miaka ya 1990 na mpaka kufikia sasa kuna maboresho mengi sana yamefanywa na juu ya kebo hizi za USB hali hii inafanya zisifanane kwa umbo, na kingine ni kwamba kuna zile ambazo zinahamisha taarifa au kuzifikisha kwa haraka zaidi kushinda zingine.

USB zipo za aina nyingi sana na bado zinaongezeka tuu, sasa labda nikuulize swali hivi unazijua aina za USB kweli? Ni wazi kuwa zipo nyingi ila leo tunakuchambulia moja moja na matumizi yake.

USB-A

USB A
USB A

Kwa jina lingine inajulikana kama USB Type- A. Hii ndio USB ya kawaida kabisa ile ambayo tumeizoea na mara nyingi na huwa tunatumia mara kwa mara katka kompyuta zetu katika kuhamisha taarifa, kutumia kama kiunganishi cha mawasiliano na exteno au hata ‘mouse’ n.k

INAYOHUSIANA  Simu janja chini ya nusu ya asilimia moja ndio zinatumia Oreo #Ripoti

USB-B

USB B
USB B

Hizi mara nyingi zinakuwa na umbo la pembe nne mraba na mara nyingi hutumika katika ‘printer’ na mara chache unakuta zinapatikana katika diski za zihada, ‘exteno’, lakini hizi sio maarufu sana kama type A

USB-C

USB-C (Type C)
USB-C (Type C)

Hizi ndio mojawapo katika aina mpya za USB ambazo zimeingia. Utofauti mkubwa na zingine ni kwamba kwanza kabisa katika kuchomekwa, hizi huwa hata ukitaka unaweza kuchomeka juu-chini na pia zina sifa kubwa ya kuhamisha taarifa kwa uharaka sana. Kingine ni kwamba hizi huwa ni ndogo sana ukilinganisha na USB za Kawaida ambazo tumezizoea na laptop, tabiti na simu janja nyingi mpya kwa sasa zinakuja na USB ya aina hii

INAYOHUSIANA  Samsung: Samsung Galaxy S10 ni familia ya simu nne! Fahamu vipya kutoka Samsung

Mini-USB

Mini USB
Mini USB

Aina hii kwa kipindi kirefu imekua ikitumika katika simu za kawaida kabisa na vifaa vingine kama vile kamera na hata MP3. Hizi pia ni ndogo ukilinganisha na USB za kawaida na ndio sababu zilikuwa  zinatumika mara kwa mara kwa vifaa vidogo. Kwa sasa hazitumiki sana ila bado utakuta kuna vifaa vingine vinatumia

Micro-USB

Mirco USB
Mirco USB

Kwa sasa hii ndio aina ambayo karibia kila mtu anaijua kwani ndio inatumika katika kuchajia simu janja nyingi sana. Licha ya kuwa na umaarufu mkubwa sana vifaa vyote vya Apple havijawahi kutumia aina hii ya USB. Uzuri mwingine wa USB hizi ni kwamba unaweza kusoma taarifa za kifaa bila kutumia msaada wa kompyuta kwa mfano unaweza ukaunganisha kifaa kwenda katika simu na ukasoma taarifa zake moja kwa moja.

INAYOHUSIANA  APPLE watambulisha iPhone 8 na simu ya iPhone X ya zaidi ya Tsh Milioni 2

USB 3

USB 3
USB 3

Kwa jina la kitaalamu zinajulikana kama ‘Backward Compatible’ ikiwa na maana kuwa zinafanya kazi kwenye USB port za zamini. USB hizi zina pini na shepu tofauti na zile za kawaida ambazo zimezoeleka.Mara nyingi hizi zinakuwa na rangi ya bluu ili kutofautisha na zile za kawaida.

Kujua Zaidi Kuhusu USB Ingia HAPA

Natumai kufikia hapa utakua umeshajua tofauti za USB na matumizi yake, kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwani daima tupo na wewe katika teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com