Ni wazi kuwa kampuni ya Netflix imeweka nia yake ya kujiingiza katika soko la magemu na nia hii iliwekwa wazi kuanzia mwaka jana.
Netflix haitaki kuwa jukwaa la kuweza ku’stream video tuu, na ili kuwezesha hili ni lazima kuongeza vitu vingine vingi na kwa upande mwingine wameona magemu ni kitu kimojawapo.
Kwa sasa mtandao huo umeinunua kampuni ambayo inajihusisha na kutengeneza magemu na kampuni hiyo inakua ni ya sita katika makampuni ambayo yanatengeneza magemu yaliyo chini ya mtandao huo.
Spry Fox inasifika sana kwa magemu ya Triple Town, Alphabear na Cozy Grove ukaichana na mengine mengi tuu. Hii inaufanya mtandao kuwa umefanya chaguo sahahi kabisa la ununuzi.
Netflix lengo lake ni kutengeneza magemu/michezo mizuri na studio nyingi ambazo inazimiliki. Ikumbukwe kuwa mtandao ulionyesha nia yake ya kuingia katika tasnia ya magemu mwezi julai 2021.
Baada ya miezi kadhaa tuu iliweza kuinunua kampuniya Night School, ikiwa ni kampuni yake ya kwanza katika hizi kampuni ambazo zinaandaa (zintengeneza) magemu.
Baada ya hapo iliachia baadhi ya magemu (kwa baadhi ya maeneo) kupitia katika App yake ya simu lakini mapokeo na ubora wa magemu hayo haukua mzuri.
Ili kila kitu lazima kiwe na mwanzo sio? Na hii ndio maana kampuni bado inahakikisha kuwa inajiongeza kupitia Nyanja tofauti tofauti ikiwemo kama hii ya kununua makampuni ambayo yamebobea katika Nyanja hii.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Na uko tayari kuanza kucheza magemu katika mtandao wa Netflix?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.