fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple IPhone

Labda Mpaka Kufikia 2023 iPhone Zitakua Na Charge Ya Type-C (USB-C)!

Labda Mpaka Kufikia 2023 iPhone Zitakua Na Charge Ya Type-C (USB-C)!

Spread the love

Fununu zinasema mpaka kufikia 2023 kwa iPhone ambazo zinakuja basi zitakua na sehemu ya kuchaji ambayo tundu lake litakua ni lile la Type-C.

Kumbuka aina hizi za chaja simu nyingi za Android ndio zinatumia. Kumbuka habari nyingi kuhusiana na iPhone na charger ya ina hii vimehusishwa sana

SOMA PIA  Huawei ya pili kimauzo kwa mara ya kwanza

Wengi wakisema ni jambo zuri na wengine wakidai kuwa sio jambo jema kuanza kuaingiliana charge na makampuni mengine ya simu.

Kumbuka asilimia kubwa sana ya soko la simu janja wote wanatumia au wameikubali teknolojia ya USB-C (Type-C) katika chaja zake.

Chaja Ya iPhone

Chaja Ya iPhone

Kuna kipindi Apple ilikua inapinga vikali chaja za aina nyingine ukiacha na chaja zao, wengine wanasema kuna muda walitaka kuchukua maamuzi magumu zaidi.

Maamuzi yenyewe ni kwamba walikua wako radhi katoa tundu la chaja kabisa na kuanza kutegemea chaja zao zile za bila nyaya.

Hakuna mambo mengi sana kuhusiana na jambo hili, lakini kama kawaida yetu tukipata za kina kabisa tutakuletea hapa hapa katika mtandao wako pendwa.

SOMA PIA  Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

Niandikie hapo chini katika eneo la comment, hii umepokeaje? napenda kusikia kutoka kwako sana wewe ambae ni mtumiaji wa iPhone…

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania