Ni wazi kuwa mtandao wa snapchat ndio mtandao ambao ulileta mapinduzi katika eneo la story katika mitandao ya kijamii, ukiachana na hayo ni wale wateja wa Snapchat Plus kuna kingine wamepatiwa.
Watumaiji wa mtandao wa kijamii wa Snapchat wale wa kulipia wameletewa vipengele vipya vingi kimojawapo kikiwa ni uwezo wa kuifanya story kukaa kuanzia lisaa mpaka siku saba.
Kinachofanyikiwa hapa ni kwamba mtu ambae ana mpango wa kuweka story hiyo atakua na mamlaka ya kuchagua muda wa snap hiyo kuanekana na chaguzi ni lisaa mpaka siku saba.
Ukiachana na kipengele hicho kuna vipengele vingine ambavyo vimeongezwa katika mtandao navyo ni sauti mpya za taarifa (notification), maboresho katika baadhi ya vipengele katika kamera.
Mabadiliko katika Bitmoji (kwa wale wanaotumia) pia yatakuwepo. Huduma ya Snapchat+ inapatikana kwa dola za kimarekani 5.99 kwa mwezi na inatoa vipengele vingi sana kwa wateja ukilinganisha na snapchat ya kawaida.
Kwa wale wanaotumia mtandao huu wa kawaida (bila kulipia) hakuna kipengele kikubwa ambacho kina mashiko kwa sasa ambacho kinapatikana katika sasisho.
Huu ni moja kati ya mitandao ambao ina nguvu sana katika jamii na ina watumiji wengi, huduma ya Snapchat+ kwa haraka haraka ina watumiji (wanaolipia) milioni 1.5 ikiwa ni namba kubwa kwani imeanzishwa mizezi kadhaa iliyopita
Kaa nasi, tutakujuza kwa lolote linalohusu mtandao huu wa snapchat, ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je vipengele hivi vinaweza kukufanya uanze kulipia huduma hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.