Movie nyingi siku hizi zinaonyeshwa kupitia huduma za ku’stream na ni wazi movie nyingi zinaenda katika mitandao mikubwa kama vile HBO Max n.k
Janga la CORONA liliathiri biashara nyingi sana hasa zile ambazo ni za mikusanyiko kama vile maswala ya kwenda katika sinema za video.
Hali hii ilipelekea movie nyingi kuonyeshwa katika mitandao ya ku’stream’ na kumekuwa na sekeseke kwamba movie zikionyeshwa katika mitandao hiyo huwa zinarudisha hela kidogo kuliko matarajio.

HBO Max na Disney Plus imekua mitandao ya ku’stream ambayo imekua ikionyesha movie nyingi sana baada ya janga la korona bila kuwasahau wakongwe, Netflix.
Waandaji wengi walipinga swala la movie kuonyeshwa katika mitandoa hii kwa kudai kuwa ile dhima ya kuangalia movie ukumbini inapotea na kwani ina ladha ya aina yake.
AMC Ambao wanamiliki kumbi nyingi sana za maonyesho, wameingia mkataba waandaaji wa movie wakongwe kabisa wanaojulikana kama Warner Bros. mkataba huu unawaladhimu waanze kuonyesha movie mpya ukumbini kwa siku 45 kwanza.
Yaani siku 45 za kwanza ni movie hizo zionyeshwe katika ukumbi na zikishapita ndio ziende katika huduma ya ku’stream.
Kumbuka Warner Bros wana movie nyingi sana ambazo zinatarajiwa kutoka mwakani, Movie kama toleo lijalo la Batman linangojewa kwa hamu sana na hapo awali walisema kuwa litaonyeshwa katika mtandao wa HBO Max.

Kwa mkataba huu inamaanisha kwamba movie itaanzia kwanza ukumbini na baadae (baada ya siku 45) ndio itaenda katika mtandao wa HBO Max.
Kumekuwa na vita kubwa juu ya nani aanze kuonyesha movie mara tuu ukitoka, je ni mitandoa hii au ni ukumbi? kumbuka mara ya kwanza ilikua unaanza ukumbi alaf baada ya siku kadhaa ndio zinaenda katika mitandao hii
No Comment! Be the first one.